![]() |
| Mwenyekiti Uvccm Mbeya Amani Kajuna akizungumza katika Mkutanao huo wa Baraza . |
![]() |
| Wajumbe wakiwa makini kusikiliza yanayojili katika Mkutano huo |
![]() |
| Katibu wa Hamasa Chipukizi Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Ndugu Paul Makonda akitoa neno la nasaha kwa wajumbe waliohudhuria mkutano huo toka Mbeya na Mikoa Mbalimbali Nchini. |
![]() |
| Katibu wa Mwenezi Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Diwani Kata ya Bagamoyo Wilayani Rungwe Ndugu Bashiru Madodi akizungumza na vijana wa jumuiya hiyo. |
![]() |
| Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Uvccm Ndugu Nwaka Mwakisu |
![]() |
| Msanii wa Bongo Movie Steven Nyerere ambaye nae ni miongoni mwa wageni walioalikiwa katika Mkutano huo pamoja na sherehe za usimikaji Makamnda 11 wa Mbeya . |
![]() |
| Mjumbe wa Baraza kuu Uvccm toka Mkoani Tanga Husna Sekiboko akitoa neno fupi kwa wajumbe wa mkutano huo. |
![]() |
| Serebuka Time |
Na EmanuelMadafa,MBEYA
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, UVCCM, umetakiwa
kuacha tabia ya kukubali kutumika na baadhi ya wanasiasa wenye uchu wa kuwania
madaraka ya urais.
Imeelezwa kuwa endapo
umoja huo utakubali ushawishi kutoka kwa wanasiasa hao iko
hatari kubwa ya jumuiya hiyo kusambaratika .
Tahadhari hiyo imetolewa
na Makada mbalimbaliwa CCM na UVCCM kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la umoja huo
Mkoa wa Mbeya uliofanyika kwa siku moja mjini hapa na kuhudhuriwa na Wenyeviti
na Makatibu wa UVCCM kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza katika
Mkutano huo wa baraza Katibu Mwenyezi wa CCM mkoa wa Mbeya, Ndugu Bashiru Madodi, amesema endapo tabia hiyo
itaendelea kuna hatari kwa UVCCM kusambaratika hata kabla ya uchaguzi mkuu ujao
hii ni kutokana na kuongezeka kwa makundi ndani ya umoja huo.
Hata hivyo Mwezi huyo
amebainisha kuwa kama watakubali hali kunauwezekano mkubwa wa jumuiya hiyo kuto
fika hata Mwezi wa Nne mwakani kama wataendelea kukumbatioa tabia hiyo .
Amesema ipo dalili kubwa
ya baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kuonyesha waziwazi juu ya kuonyesha wazi
kujikita katika kundi Fulani la watu wanao taka kuingia Ikulu.
Amesema watu hao wanaotangaza
nia wanawafuata kwa sababu wanajua kuwa bila ya kuwashirikisha vijana hao kamwe
hawezi kufanikisha malengo yao kwa sababu ya vijana kuwa na nguvu ndani ya chama hivyo amewataka kuwa makini kwa kutumia nguvu na ushawishi wao vizuri.
Naye Katibu wa
Hamasa wa UVCCM Taifa, Paul Makonda, amesema tatizo kubwa linaloukabili uomoja
huo kwa sasa ni uwepo wa wanachama wasiojitambua kisiasa ambao wamekubali
kuwekwa mifukoni na wanaotaka kuingia Ikulu hali inayosababisha kukosa ujasiri
katika matendo na kauli zao na hivyo kila wanalolifanya lazima waseme wametumwa
na fulani.
Mwenyekiti wa UVCCM
Mkoani Mbeya, Amani Kajuna, amesema vijana wanapaswa kusubiri maamuzi ya chama
kuhusu mgombea atakayeipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi ujao na kuunga
mkono uamuzi huo badala ya kujiingiza kwenye makundi yanayohatarisha uhai wa
umoja huo.
Amesema umoja mshikamano ndio utakawezesha chama kupata kiongozi bora anayehitajika pamoja na kuendelea kukipa nguvu chama.
Mjumbe wa NEC Zanzibar,
Nadya Juma Mohammed, amewataka vijana kutambua kuwa harakati za uchaguzi
zinazohatarisha uhai wa UVCCM ni tukio la kipindi kifupi hivyo wanapaswa kuwa
makini na wasikubali kugawanywa na wanasiasa hao kwa sababu uhai wa umoja huo
unahitaji nguvu yao ya pamoja kwa muda mrefu.
Wakizungumzia sakata la
Ukawa,Katibu wa CCM Wilaya ya Ileje, Luciano Mbossa , aliwataka vijana wa
CCM kupambana na kundi la Ukawa kwani ndio saizi yao na kuwaachia wazee wa CCM
kutangaza ilani ya chama na utekelezaji wa sera kwa wananchi.
Hata hivyo, akifungua
mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Godfrey Zambi, aliwataka UVCCM
kutokubali kununuliwa na wanasiasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
mkuu ili kuepusha kupitisha wanasiasa wasiokuwa na uwezo.
Mwisho


















Post a Comment