Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye  kilele cha Sherehe za Miaka 75 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa tuzo na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 75 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha  Tanzania Assemblies of God (TAG) akiwa na  Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 75 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014.PICHA NA IKULU
Na EmanuelMadafa,mbeya
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ametoa pongezi kwa viongozi wakuu wa vyama vya kisiasa nchini kwa hatua yao ya kukutana na kujadili mskabari wa maendeleo ya upatikanaji wa katiba mpya.

Kikwete amesema hayo  hayo leo jijini Mbeya  , wakati akihutubia kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75  tangu kuasisiwa na kuanzishwa kwa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)  na kufanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini hapa.

Viongoiz walikokutana ni pamoja na mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi Ccm ,Chadema ,Nccr mageuzi,na Cuf.

Amesema hatua ya ya viongoizi hao wakuu wa vyama  vya kisiasa kukutana kujadili suala hilo ni hatua nzuri na inapaswa kuungwa mkono na wote sanjali na kutoa fursa kwao  ili waweze kufikia muafaka wao.

Amesema, matumaini ya watanzania wote ni kuhakikisha Katiba hiyo mpya inapatikana kwa wakati ikiwa imeweka bayana  nchi kuongozwa kwa serikali mbili au tatu.

Jakaya, alilazimika kulizungumzia hilo baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Tanzania, Dr. Barnabas Mtokambali, kumuomba Rais kuingilia kati suala la mchakato wa upatikanaji wa katiba hiyo kutokana na baadhi ya wajumbe kuweka msimamo wa kutorejea bungeni kutokana na kupishana kwa mitazamo wakati wa kujadili sura ya kwanza na yapili ya rasimu hiyo.

Aidha Rais Kikwete amesema kuwa amefarijika  kusikia  viongozi hao na waumini wa kanisa hilo wakiendelea kuwasihi wajumbe hawa ambao waliondoka Bungeni kurejea  kwani  matumaini ya wote ni kumalizika kwa kazi hiyo  ambayo kwa asilimia kubwa tayari imemalizika.

Amesema, Katiba hiyo mpya  imelenga kuondoa au kumaliza kasoro ndogondogo zilizomo kwenye katiba ya awali ambayo inatumika sasa hivyo ni vema wajumbe wakaliona hilo na kuwatendea haki wananchi ambao wanawawakilisha.

Aidha, Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwaondoa wasiwasi watanzania  ambao baadhi wameonyesha kukata tamaa na upatikanaji wa Katiba hiyo mpya kwa wakati kwani tayari pande hizo zimeanza meza ya mazungumzo hivyo   anamatumaini makubwa na wajumbe hao kurejea Bungeni ifikapo Mwezi Agosti ikiwa ni awamu ya pili ya wajumbe kujadili Katiba hiyo .

 Pia, katika kusisistiza hilo Rais, aliwaomba waumini na wachungaji wa madhehebu mbalimbali kuendelea na maombi ya kuwaombea wajumbe hao kuondokana na mapepo ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakichangia kuvuruga amani iliyopo ndani ya Bunge hilo.

Kadhalika, Kikwete amewataka viongozi hao wa dini kuendelea na kazi yao ya kuhubiri amani na upendo nchini , kwani hali hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya uhalifu na uovu vilivyojikita ndani ya jamii na kuipunguzia serikali mzigo.

mwisho

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top