STAA wa filamu Bongo, Riyama Ally amesema katika maisha yake
hajawahi kumtukana mwanaume pindi anaponitokea hata kama hamuhitaji, anamjibu
kwa busara.
Akipiga stori na paparazi wetu, Riyama alisema yeye yupo tofauti
na wasichana wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuwatukana wanaume pindi
wanapowasilisha hisia zao za kimapenzi kwa sababu tu hawavutiwi kuwa nao.
“Hata kama mtu akinitongoza na nikawa simuhitaji kamwe siwezi
kumtukana wala kumuonyesha dharau , kimaadili sisi sote ni binadamu na kila mtu
ana hisia zake na maamuzi yake, namjibu tu kistaarabu kwamba mimi nina mtu
wangu, kumjibu mwanaume vibaya Mungu hapendi,” alisema Riyama.







Post a Comment