Na Boniface Wambura, Johannesburg
Kikosi cha Taifa Stars
kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya
maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi
ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni
kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho
asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
Wakati huo huo, Balozi
wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea
timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.
Serengeti Boys yenyewe
ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa
Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).







Post a Comment