Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Daktari Mohamed Kiholile akizungumza katika moja kikao cha wadau wa Mfuko wa CHF Kilicho wahusisha wadau Mbalimbali wakiwemo wakuu wa Wilaya na vingozi wa Mkoa sanjali na waganga wakuu

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Daktari Sefu Mhina 
Baadhi ya wakuu wa Wilaya


Na EmanuelMadafa,Mbeya
Viongozi Wakuu wa Mkoa na Wilaya Mkoani Mbeya wamekutana jijini Mbeya na kuweka maadhimo kadhaa yatakayo uwezesha Mfuko wa Afya jamii CHF kufikia malengo yake   ya asilimia 30 ya wananchi kujiunga na mfuko huo  mara ifikapo mwezi Desemba Mwaka huu.

Wadau hao ni pamoja na Wakuu wote wa Wilaya Mkoani Mbeya , Wakurugenzi wa Halmashauri na sanjali na viongozi wa Mkoa wa Mbeya pamoja na waganga wakuu .
Akitoa maadhimio ya Mkutano huo Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Daktari Mohamed Kiholile amesema kuwa  katika mkutano wakuu  hao wameweka maadhimio 17 ambayo yatatakiwa kutekelezwa na  Mfuko huo wa Taifa NHIF kwa kushirikiana na viongozi hao .

Amesema moja ya Maadhimio hayo ni pamoja na  kuhakikisha kuwa halmashauri zote za mkoa huo zinaimarisha  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba  sanjali na  kuongeza usajili wa wanachama  kwa kuwahusisha  waratibu kata elimu na wakuu wote wa shule.

Amesema adhimio jingine ni  kuhakikisha kuwa kila halmashauri inajiwekea mikakati ya  kuwapiga picha wanachama wapya wa CHF kwa lengo la kupunguza gharama  hali ambayo itachangia kwa wao kuwahamasika  kujiunga na Mfuko huo.

Hata hivyo  Meneja huyo wa Bima ya Afya amesema kuwa wadau hao pia wameutaka mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF  kuhakikisha inafanya  mchakato wa haraka wa ubadirishaji wa sheria ya CHF sanjali na utoa wa taarifa kwa wadau hao juu ya wapi wamefikia katika mchakato huo.

Pia amesema kuwa mkakati mwingine uliwekwa na wadau  hao ni kuhakikisha kuwa  kila wanapokutana  wanapeana mrejesho wa maadhimio yaliyopita sanjali na utekelezaji wake.

mwisho


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top