![]() |
| Baadhi ya wachungaji wa wa kanisa hilo wakiwa makini kumsikiliza Askofu Mkuu wa Kanisa hilo. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) anatalajiwa kuongoza wachungaji wapatao 8000 kutoka Maeneo Mbalimbali Nchini
kwa ajili ya shughuli ya uchangiaji Damu Katika kituo cha damu
salama Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mbeya.
Akizungumzia hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Dr. Barnabas
Mtokambali, amesema wachungaji hao wakiongozwa nayeye mwenyewe watachangia
damu hiyo kwa hiari lengo kuu likiwa ni kuokoa uhai wa watu ambao hupoteza
maisha kutokana na kupungukiwa damu.
Amebainisha kuwa kundi la
kinamama wajawazito,watoto na majeruhi wa ajali wamekuwa wanahitaji damu nyingi
mara wanapopata matatizo ya maradhi na ajali hivyo ni vema wao wakajitolea ili
kupunguza idadi ya vifo hivyo.
Aidha, Askofu Mtokambali, amesema zoezi hilo litaanza na
wachungaji 800 ambapo kama mungu atakuwa amesaidia wahusika wote wakakidhi
vigezo na masharti basi benki ya damu itakuwa imepokea lita 400.
Amesema, wachungaji wengine 4500 kutoka maeneo mbalimbali ya ndani
na nje ya nchi wataungana na wenzao kwenye zoezi hilo mara watakapokuwa
wamewasili.
Amesema, tayari kanisa limefanya taratibu zote za mawasiliano na
ofisi ya Kanda kitengo cha Damu Salama kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na
kwamba zimekamilika.
Hata hivyo, amewaomba wahusika wa kitengo hicho kujipanga vizuri
kwani matumaini yake ni kwamba mbali na wachungaji hao wapo baadhi ya watu
ambao nao watahitaji kuunga mkono zoezi hilo hivyo ni vema wakajipanga vizuri
kwa vifaa pamoja na watoa huduma.
Mwisho.











Post a Comment