Meya wa jiji la Mbeya Atanas Kapunga akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mara baada ya kukutana na ujumbe wa NHC. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Shirika la nyumba la Taifa
NHC limekubali kutoa timu ya wataalam watakaosaidiania na Halmashauri ya jiji
la Mbeya katika suala zima la uchoraji mpya wa ramani (MasterPlan) itakayotumika kwa
ajili ya ujenzi wa makazi mapya katika halmasahuri ya jiji la mbeya.
Kauli hiyo imetolewa na Meya
wa jiji la Mbeya Ndugu Athanas Kapunga mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo
na ujumbe wa shirika hilo uliotembelea katika maeneo mbalimbali ya miradi
inayotalajiwa kutekelezwa na shirika hilo la NHC.
Kapunga amesema mara baada
ya kukutana na ujumbe huo ambao umeongozwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Ndugu
Nehemia Mchechu umelidhia kupeleka timu hiyo ya wataalam ambayo inashirikiana
moja kwamoja na wataalam wa halmashauri hiyo ya jiji la mbeya katika
kutengeneza mpango huo.
Aidha amesema timu hiyo
itaingia jijini humo mapema mwezi Octoba mwaka huu ili kuanza mkakati huo kwa kuanza na hatua ya
utoaji wa semina kwa wataalamu hao wa jiji la mbeya hususani katika idara ya
mipango miji.
Amesema maeneo ambayo
yatapewa kipaumbele katika utekelezaji wa shughuli hiyo ni pamoja na eneo la Iwambi
ambalo liemegaiwa kwa wakazi wa jiji la mbeya pamoja na eneo la stendi kuu ya
mabasi jijini humo.
Hata hivyo Ndugu Athanas
Kapunga ameweka wazi juu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa soko jipya la kisasa
katika eneo la Uhindini ambalo nalo ujenzi wake utakuwa chini ya shirika hilo
la nyumba NHC.
Mwisho.
Post a Comment