Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

 Katibu Mkuu wa CCM, ADULRAHMAN Kinana akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA aliposimama kwa muda akitokea ziara ya Kisiwa cha Mafia kwenda Dar es Salaam. Alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kitendo cha kuanzisha shule hiyo yenye manufaa makubwa kwa watoto ya kike wanaotoka sehemu mbalimbali nchini kwenda kusoma hapo. Pia alitumia furssa hiyo kuwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanaoifanya kiasi cha kufanikisha wanafunzi kufanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkuu wa shule hiyo, Suma akielezea historia ya shule hiyo inayojuisha watoto wengi yatima
 Wanafunzi wakifurahia pongezi za ufaulu mzuri zilizotolewa na Kinana
 Moja ya majengo ya shule hiyo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaimbisha wanafunzi wa shule hiyo wimbo wa 'Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote', uliotungwa enzi hizo na babake Moses Nnauye.
Wanafunzi wakishangilia kwa furaha baada ya kuimba bila matatizo wimbo huo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top