Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Jeshi la Polisi Mkoani   Mbeya linawashikilia wahamiaji haramu sita kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Watu hao ni pamoja na   Zinabu Asseta (29) r Kadeh wahalu (27) ambao ni raia  ethiopia .

Wengine ni  Jackquline Uhasi (07) beatha (30)   oliver (25)  raia na mkazi wa nchini kongo  devine (25).
              
Wahamiaji hao walikamatwa Septemba 14 mwaka huu majira ya saa 2 usiku huko katika kijiji cha  mkola wilayani  ya Chunya, mkoani humo .
     
Wahamiaji hao walikamatwa wakiwa wanasafirishwa kwenye basi t.791 acj aina ya scania mali ya kampuni ya super service. Taratibu za kuwakabidhi idara ya uhamiaji zinaendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Ahmed  Msangi anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaowatilia mashaka katika maeneo yao ili uchunguzi ufanywe dhidi yao na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Mwisho.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top