Na Mwandishi wetu,Iringa
WATALII kutoka nchi ya Ujerumani, wamestaabishwa na
maajabu ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa, kutokana na kuwa na
Tembo pamoja na Simba wenye maumbo makubwa huku wakitembea kwa makundi.
Wamesema, licha ya kubahatika kutembelea mbuga mbaimbali katika
nchi za Afrika, hawajawahi kukutana na mnyama aina ya Tembo pamoja na Simba
wakiwa na maumbo makubwa huku wakishangazwa na uwezo wa Simba wa kuua Tembo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mtalii, Maik Zobel kutoka
nchini Ujerumani, alipotembelea hifadhi hiyo ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani
Iringa.
‘’Nimeshuhudia Simba wakiwa wamemuua tembo mkubwa katika hifadhi
hii na wanatembea kwa makundi na hili ni jambo la ajabu sana kwangu,kiufupi
nimeona wanyama wengi sana katika hifadhi hii’’alisema Zobel.
Aidha, Mtalii huyo hakusita kuimwagia sifa Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha, kwakua na utulivu mkubwa hali inayo wawezesha watalii kuwaona
wananyama na ndege wa aina mbalimbali bila ya kusafiri umbali mrefu kuwatafuta.
Hata hivyo Maik Zobel alitoa witoa kwa serikali ya Tanzania
kuongeza usimamizi madhubuti wa kuhakikisha wanawahifadhi wanyama na uoto wa
asili katika maeneo ya hifadhi kwa ghamara yoyote ile kwajili ya urithi wa
vizazi vijavyo.
Kwa upande wake, Afisa Mwandamizi wa hifadhi hiyo ya Taifa ya
Ruaha,Eva Pwelle, alisema uongozi wa Hifadhi hiyo, unaendelea na jitihada
za kuimarisha miundombinu ya barabara na maeneo ya kulala wageni
katika hifadhi hiyo.
Aliyataja baadhi ya maeneo yatakayoimarishwa kwajili ya
kulala wageni ni ujenzi wa Mahema,mabanda ya Msonge,mabweni pamoja na nyumba
ndogo katika maeneo mbalimbali ya hifadhi.
mwisho
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment