Kamanda wa Polisi mbeya Ahmed Msangi |
Na EmanuelMadafa,mbeya
MAHABUSU aliyefahamika kwa jina la Andaluswe Mwakapila (60)
mkazi wa Ilongo Wilayani Mbarali mkoani Mbeya amejinyonga na kupoteza
maisha akiwa ndani ya mahabusu.
Akielezea tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi
amesema tukio hilo limetokea juzi, alifajili kwenye mahabusu iliyopo
katika kituo kidogo cha polisi cha Inyala kilichopo katikA Wilaya ya kipolisi
ya Mbalizi Mkoani Mbeya.
Amesema, marehemu huyo alikutwa amepoteza maisha ndani ya mahabusu
hiyo huku mwili wake ukiwa umening’inia kwenye dirisha dogo la chumba hicho.
Msangi, akifafanua kutokea kwa tukio hilo, amesema marehemu huyo
akiwa ndani ya chumba chake cha mahabusu inadaiwa alijinyonga kwa kutumia shati
lake.
Amesema, askari wa zamu waliingia ndani ya chumba hicho ikiwa ni
moja ya utaratibu wao wa kukagua na kushuhudia mwili wa mzee huyo ukiwa
umening’inia juu na shingoni kwake kukiwa kumefungwa shati lililofungwa kwenye
dirisha dogo la chumba hicho cha mahabusu.
Amesema, askari hao waliuchukua mwili wa marehemu huyo na
kuufikisha katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo ulifanyiwa uchunguzi na
kubainika kwamba marehemu alijinyonga.
Hata hivyo, Kamanda Msangi, alisema marehemu alikuwa
akikabiliwa na kosa la kumdhulu mke wake kwa kumpiga kwa vitu vyenye ncha
kali hali iliyosababisha kupata majeraha makubwa kichwani.
Aidha uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa na ugomvi
na mke wake ambapo alimpiga kwa kutumia shoka na jembe hivyo kumsababishia
majeraha kichwani na kwamba hali ya mama huyo inaendelea vizuri katika
hospitali ya Rufaa.
Mwisho.
Post a Comment