Na Boniface Wambura
Makocha 35 wameteuliwa kushiriki kozi ya
ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika
mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
Kozi
hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia Mchikichini
College ambapo washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya
ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na vyeti vya kitaaluma vya elimu ya
sekondari (academic).
Washiriki
wa kozi hiyo ni Abdulmaliki Nemes (Airport FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro
Talented Youth Sports Centre), Ally Jangalu (Moro Kids), Amri Saidi (Mwadui
FC), Athuman Kambi (Morogoro), Charles Mwakambaya (Burkina Faso FC), Damian Mussa (Alliance One) na
Daudi Sichinga (Kasulu United).
Denis Maneva (Shule ya Msingi Logo), Edgar
Juvenary (JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya Msingi Mtimbwilimbwili),
Henry Ngondo (Chalinze Academy), Issa Hamisi (Polisi Kilimanjaro), Jumanne
Chale (Dar es Salaam), Kizito Mbano (Masasi Alliance), Martin Saanya (Magereza
Morogoro) na Masoud Gumbwa (Sokoine University Academy).
Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage Kabange
(Kagera Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC), Nsubuga Solomon (Kishoto FC),
Nyamtimba Muga (Kizuka Secondary), Oscar Mirambo (Makongo), Rashid Abdallah
(Tech Fort Academy), Renatus Shija (Rhino Rangers), Safari Nyerere (Elimu
Sports Academy) na Said Lyakuka (Kizuka Stars).
Simeon
Mwesa (Mtibwa Sugar U20), Simon Shija (Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu
Shooting), Swalehe Allawi Abdul (Alliance Academy), Yasin Bashiri (Kick Off
Sports Academy) na Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar).
Wakati
huo huo, kutakuwa na kozi ya wiki mbili ya ukocha ya ngazi ya Kati
(Intermediate) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 29 mwaka huu.
Makocha
wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha
Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).
Mwisho
Post a Comment