Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri Lazaro Nyalandu akizindua kampuni ya Utalii Sept 16, 2014 jimbo la California kampuni inayomilikiwa na Balozi wa heshima Ahmed Issa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Mbeya

  Na Emanuel Madafa, Mbeya.
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, Waziri  wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, aibuka na kufafanua tuhumza zinazomkabili dhidi yake na msanii wa  filamu Tanzania Aunty Ezekiel na kudai kuwa hazina ukweli wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Nyalandu ambaye alikuwa anapita kuelekea mkoani njombe kwa kazi ya kumsimika Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Njombe, tuhuma hizo hazina ukweli wowote zaidi zimelenga kumchufua kutokana na utendaji kazi wake.

Anasema, safari yake nchini Marekani  ilikuwa ni kufungua tamasha la Utamaduni na Utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ikiwemo kuwatangaza wasani  kimataifa lililoendeshwa na Blog ya Vijimambo lililofanyika September 13.

Anasema, alifika nchini Marekani siku ya Ijumaa Sept 12 kwa lengo moja la kuzindua tamasha la Utalii na kutoa vyeti kwa washiriki wa tamasha hilo na kwamba Aunty Ezekiel na msanii mwingine wa Bongo Flava Kassim Mganga  waliingia nchini humo September 13 na kwamba safari zao ziliratibiwa na Kamati nzima ya Vijimambo kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani.

Anasema,  yeye pamoja na msanii huyo walionana mara moja tu, tena usiku wa tukio ambalo lilifanyika Sept 13, 2014 kwenye kilele cha sherehe ya Utalii na baada ya hapo hawakuwahi kuonana tena na baada ya sherehe ya Utalii Jumatatu, Nyalandu alisafiri kuelekea California kuzindua kampuni ya Utalii ya Tanzania Safari and Tourism inayomilikiwa na Balozi wa Heshima Ahmed Issa na hakuwahi kurudi tena Washington, DC mpaka siku aliyoondoka.

“Sikuwahi kutanua na msanii huyu kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari lakini si shangai kwani mambo haya yamekuwa yakifanywa na genge la watu ambao miongoni mwao ni viongozi wa serikali tena waliomo kwenye Wizara yangu,”alisema.
Anasema,  lengo la habari hiyo ni kuendelea kutimiza mikakati ya kumchafua kwani haina ukweli wowote.

Hata hivyo Waziri huyo alisema, tayari amewatambua watu hao nakwamba yeye ataendelea na msimamo wake wa kulinda maslahi ya taifa hususani katika nafasi yake hiyo huku akisisitiza kuwa hato thubutu kushawishika na magenge hayo kwa lengo la kuregeza kamba.

“Rais aliponiteua kwa mara ya kwanza kushika nyadhifa hii, kunagenge la watu lilinifuata na kunitaka kuendelea kushirikiana nao katika kuihujumu nchi kwa kuwaua tembo na kusafirisha nyara za serikali nje ya nchi jambo ambalo nililikataa,”alisema.

Amesema, kitendo cha kutokubaliana na matakwa ya watu hao ndi chanzo cha kutengenezewa mizengwe hiyo hadi kufikia hatua ya kutafutiwa skendo skendo na kama wangeipata  basi lazima ingeandikwa, ila ninaloweza kusema sitajiunga na genge lolote  ambalo lengo lake ni kuangamiza rasilimali za tanzanaia. 

“Kuna watu wamekaa pembeni kumuona Nyalandu akianguaka lakini ningependa kuwaeleza kuwa huwezi kumuangusha mtu anayesimamia haki kwa kumchafua kupitia vyombo vya habari , haya yote ni mapambano yanayofanywa au kutekelezwa na kundi la majangili ambalo ndani yake wamo watendaji wa serikali na wanasiasa,”anasema.

Amesema, haingii akilini kiongozi wa serikali kutumia fedha ya serikali eti kwenda kutanua na msanii wa Filamu Aunt Ezekieli Marekani huo ni uzushi ambao umevuka mpaka, ni vema wahusika wanaoeneza uvumi huo kutambua kuwa nchi haiendeshwi kwa kukumbatia watu waongo, wafitini, majungu na wenye hila.

Waziri Nyalandu, alimaliza kwa usemi usemao “Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni”, siwezi kukubali au kulilihusu kundi hili la majangili kudhorotesha uchumi wa Taifa kwani maneno au tuhuma hizo haziathiri utendaji kazi wake  bali kumuongezea kasi katika ufanisi wa shughuli za maendeleo hususani utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo imelenga kuwaletea wananchi maendeleo na maisha bora.
  
Amesema, suluhisho ni viongozi na wananchi kufanya kazi kwa bidii kwa nia ya kuleta maendeleo, jambo analomshukuru Mungu kadiri siku zinavyokwenda ndio baadhi ya wananchi na viongozi wanatambua yeye hana tatizo na wao bali ni utekelezaji wa majukumu ambayo serikali imemtuma kuyafanya.

mwisho

















Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top