Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Na Emanuel Madafa, Mbeya.
ASKARI polisi wa kitengo cha usalama barabarani Wilayani Chunya
Mkoani Mbeya, PC Zeferin Didas Focas(34)
kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya mwananchi Abisai Wadi (22).
Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi,
amethibitisha kufukwa kazi kwa askari huyo baada ya husika na mauji ya raia
huyo yaliyotokea juzi katika Kata ya Igalula barabara ya Itindi /Mkwajuni Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Amesema, askari
huyo akiwa na mwezie aliisimamisha pikipiki iliyokuwa imempakia abiria nyuma
ambapo dereva huyo alikaidi, ndipo askari huyo alichukua jiwe na kuitupia
pikipiki hiyo iliyokuwa katika mwendo kasi na kumpata abiria huyo.
Amesema, jiwe hilo linasemekana lilimkuta abiria
aliyepakizwa kwenye poikipiki hiyo lakini haikuwekwa wazi kwamba jiwe hilo
lilimpata katika sehemu ipi ya mwili wa marehemu huyo.
Amesema, askari huyo ambaye kwa sasa anatambulika kwa
namba ya X6710 anatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma za mauji zinazomkabili mbele
yake.
Mwisho.
|
Post a Comment