Na EmanuelMadafa,mbeya
Hatimaye aliyekuwa askari polisi wa kitengo cha usalama
barabarani Wilayani Chunya Mkoani Mbeya, X6710 Zeferin Didas, amefikishwa
mahakamani kwa kosa la kuua bila ya kukusudia kinyume cha kifungu kidogo
cha kwanza cha sheria namba 195 na kanuni ya adhabu namba 198 sura ya 16 ya
mwaka 2002.
Akisomewa mashitaka hayo
na wakili wa serikali,Magreth Mahundi, mbele ya hakimu mkazi Batulaine
Maria, alisema askari huyo alitenda kosa hilo November 17,mwaka huu
katika eneo la Itindi Mkwajuni Wialayani chunya Mkoani Mbeya.
Amesema, mshitakiwa huyo
alidaiwa kumpiga jiwe na kumsababishia kifo marehemu Abisai Wadi (22) mkazi wa
Chunya ambaye alikuwa amepakiwa kwenye pikipiki maharufiu kama
(bodaboda).
Imeelezwa kuwa askari
huyu, akiwa katika majukumu yake ya kila siku, aliisimamisha pikipiki
hiyo iliyokuwa kwenye mwendo kasi lakini inadaiwa kuwa dereva wa bodaboda
hiyo alikakaidi agizo hilo ndipo askari huyo alipoamua kuchukua jiwe na
kumrushia na kumpata abiria na kusababisha kifo chake.
Aidha, hakimu wa
mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Mbeya, Batulaine, ameiahirisha kesi hiyo
kutokana na ushahidi kutokamilika mpaka itakapotajwa tena Desember 10 mwaka
huu.
Hata hivyo, wakili wa
utetezi wa kesi hiyo Radlsaus
Lwekazaa, tayari amepeleka
maombi ya kupatiwa mdhamana kwa mteja wake katika mahakama kuu.
Amesema Mshitakiwa
anahaki ya kuwekewa mdhamana kwa sababu ameua bila ya kukusudia hivyo tayari amewasilisha
ombi kwenye mahakama kuu ili mteja wangu apatiwe mdhamana kwani ni haki yake
kisheria.
Mwisho.
Post a Comment