Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Wananchi wa Kijiji cha Nanyanga wamerudisha kadi za CUF na kumkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kuchoshwa na dharau walioonyeshwa na Kiongozi wao mkubwa Maalim Seif baada ya uamuzi wake wa kutosimama kijijini hapo kuwapa pole wanakijiji walioezuliwa paa zao na mvua ya upepo iliyonyesha usiku wa kuamkia jana (27 Novemba).

Katibu Mkuu huyo wa Chama cha CUF amelaumiwa na wananchi hao kwa kutokuwa na msaada katika maendeleo yao wala kushiriki  pale wanachama wao wanaokuwa na shida .

Wananchi hao walimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kadi zaidi ya 100 ambaye licha ya kuwapa pole waliopata maafa aliahidi kuwasaidia ili waweze kuezekea nyumba zao

Wananchi wa kijiji cha Nanyanga wameshanga kuona kiongozi wao wa CUF akipita bia kusimama kwenye eneo la tukio, mmoja wa wanananchi hao aliyejitambulisha kwa  jina la Namaneha alisema "siamini nachokiona yaani leo Seif ameshindwa kuonyesha utu kwa kutupa angalau pole? kweli wanasiasa wengi wanaangalia maslahi yao na kutwa kupita kutulaghai kura yangu hawaipati tena"
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia moja ya nyumba zilizoathirika na mvua ya upepo kijijini Nanyanga wilaya ya Tandahimba.
 Paa la nyumba ya Ndugu Abdala Athumani Mwatama likiwa chini baada ya kuezuliwa na mvua kubwa ya upepo iliyonyesha katika kijiji cha Nanyanga wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.
 Moja ya nyumba iliyoathirika na mvua
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi juu zilizorudi kutoka upinzani

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top