Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akizindua rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Mwasisi na Rais wa Taasisi ya Hearing, William Austine, baada ya uzinduzi wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimshuhudia Mwasisi na Rais wa Taasisi ya Hearing, William Austine akimvisha mashine maalum ya kuwawezesha kusikia, mwanafunzi Amina Athuman wa darasa la tatu katika shule ya msingi Buguruni wakati wa uzinduzi utoaji wa huduma hiyo kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uliofanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha Nishani, Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Buguruni, mwenye ulemavu wa kusikia (kiziwi) , Amina Athuman, baada ya kuvishwa kifaa maalum kinachomwezesha kusikia, wakati wa uzinduzi rasmi wa utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi). Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR
 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha mwanafunzi mlemavu wa kusikia (kiziwi) Bertha Samwel wa darasa la tatu Shule ya msingi Buguruni, Kifaa maalum cha kumwezesha kusikia, wakati wa uzinduzi rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi). Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Kulia ni Mwasisi na Rais wa Taasisi ya Hearing, William Austine. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jasmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mwasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing, William Austine, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa kusikia, wakiopatia mashine maalum za kuwawezesha kusikia, baada ya kuvishwa mashine hizo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo. Picha na OMR

 Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, (Viziwi) wakisubiri kupatiwa huduma hiyo wakati wa uzinduzi.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoa huduma wa Taasisi ya Starkey Hearing. Picha na OMR

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top