Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mtoto
mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetambulika kwa jina la Angel Ramadhani amefariki dunia baada ya
kutumbukia kwenye kisima kilichopo jirani na nyumba yao.
Tukio
hilo limetokea Novemba 26 mwaka huu majira ya saa
15:30 jioni maeneo ya Ikuti, Kata ya Iyunga, jiji Mbeya.
Inadaiwa
kuwa, mtoto huyo alitambaa kuelekea kwenye kisima hicho na ndipo alipotumbukia
na kupelekea kifo chake.
Aidha,
wakati tukio hilo linatokea mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa jikoni anapika na
kumuacha mtoto huyo akiwa anacheza na ndipo alitambaa na kutumbukia kwenye
kisima kilikuwa jirani na nyumba yao.
Ambapo
tayari Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya.
Kaimu
kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi wa Polisi Barakael Masaki anatoa wito kwa wazazi na walezi
kuweka uangalizi wa kutosha kwa watoto wadogo ili kuepuka madhara yanayoweza
kujitokeza.
Aidha,
anatoa wito kwa jamii kufunika visima pamoja na vyoo sanjali na kufukia mashimo yenye maji kwani ni hatari kwa
watoto wadogo hasa katika kipindi hiki cha mvua.
Mwisho.
Post a Comment