Katibu wa Mbeya City Emanuel Kimbe |
Hatimaye Klabu ya Mbeya City imeweka bayana kuwa
bado itaendelea kushirikina na Kocha Jumma Mwambusi katika kukionoa kikosi
hicho cha Mbeya licha ya taaraifa za awali kuelezwa kuwa kocha huyo huenda
ikawa mwisho wake wa kuikonoa kikosi hicho kutokana na kuatangaza kwakwe
kujiuzulu .
Akizungumzia sakata hilo Katibu wa Klabu hiyo
ya Mbeya City inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara Emanuel Kimbe amesema Mwalimu
Juma Mwambusi ni muajiriwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya anayesimamia benchi
la ufundi la timu hiyo.
Amesema Menejiment ilikutana na Mwl Juma
Mwambusi katika vikao vyake vya kawaida kupitia changamoto kadhaa
zilizojitokeza katika michezo saba ya awali mara baada ya kuwasilisha ripoti ya
maendeleo ya timu.
Ameweka wazi kuwa Mwalimu Mwambusi na
menejiment kwa pamoja wamelidhiana kwa faida ya mpira wa miguu na jamii
inayoizunguka timu hiyo
Amesema Mwambusi ndiye Kocha Mkuu wa timu na kwa sasa anandaa program ya mafunzo kwa mzunguko
wa pili wa ligi unaotarajia kuanza disemba 2014.
MASLAHI YA WACHEZAJI
Hivi
karibuni baadhi ya wadau wa mchezo wa mpira wa miguu wamehusisha matokeo ya
uwanjani iliyopata timu na maslahi kwa wafanyakazi wa klabu kama taasisi.
Sehemu
kubwa ya wafanyakazi wa klabu ikijumuisha timu ni wafanyakazi chini ya masharti
ya mkataba chini ya muajili ambaye ni Halmashauri ya jiji la Mbeya, Hivyo
maslahi ya mfanyakazi(kwa kada hii) hujadiliwa na kukubaliana kwa pande zote
mbili(Klabu kwa niaba ya muajiri na Mchezaji kama muajiriwa) kulingana na bei
ya soko ndipo mkataba husainiwa.
Klabu
imeweka utaratibu wa namna ya wafanyakazi wake kujadiliana na mwajili kuhusu
mambo mbali mbali yenye lengo la kuboresha utendaji wa kazi na mazao yake
pamoja na masuala ya maslahi pindi kukiwa na haja hiyo.
Mishahara
ya wachezaji pamoja na kuamuliwa kwa makubaliano baada ya majadiliano ya pande
zote mbili pia bei ya soko huangaliwa na kuzingatiwa. Msimu wa 2014/2015
mishahara ya wachezaji ilipanda kati ya asilimia 100 – 300(%) ikilinganishwa na
msimu uliopita 2013/2014.
Posho
zote zitolewazo na klabu zilirekebishwa ikilinganishwa na msimu uliopita kwa
kuzingatia makubaliano kati ya wachezaji na menejimenti kabla ya kuanza kwa
msimu huu.
Klabu
inatambua wazi kuwa mpira ni ajira kama zilivyo ajira zingine,maslahi haya
yamewekwa kwa makusudi ili kuboresha hali za maisha za wafanyakazi wetu hasa
wachezaji kwani hiyo ndiyo ajira yao.
Ukiondoa
mshahara unaoendelea kulipwa kila mwezi hakuna mfanyakazi yeyote anayedai
chochote kati ya maslahi yake.
FEDHA ZA WADHAMINI:
Pamoja
na kuwa na kipengele cha kutotoa siri (Confidentiality)za mikataba yetu na
wadhamini wetu, klabu inasikitishwa namna ambavyo umma wa wanamichezo
unavyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa changamoto ambazo klabu
inapitia hivi sasa kama taasisi zinatokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini.
Klabu
inaomba ikumbukwe kuwa katika msimu uliopita 2013/2014 ilitumia zaidi ya
shilingi milioni 700 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri
ikiwa kama mmiliki wa klabu. Wadhamini kwa mujibu wa makubaliano hawajatoa wala
hawatoi fedha zote mara moja kwa mujibu wa mkataba, fedha hizo hutolewa kila
mwezi na kwa awamu.
Matumizi
ya kawaida ya klabu kwa mwezi si chini ya shilingi 49,000,000.00(bila kuhusisha
mishahara), katika kipindi cha Julai-Sept 2014, Klabu ilikuwa na mdhamini mmoja
tu ambaye ni Binslum tyres Co Ltd anayetoa shilingi 15,000,000.00 kwa mwezi
sawa na shilingi 180,000,000.00 kwa mwaka kwa mujibu wa mkataba uliopo.
Ukiangalia
mahitaji ya klabu kwa mwezi mmoja hapo juu, fedha hizi za mdhamini zilichangia
asilimia 30.6(%) ya gharama za klabu kwa mwezi. Hii ikiwa na maana kuwa bado
asilimia 69.4(%) ya gharama za uendeshaji wa timu zilitoka Halmashauri.
Kuanzia
mwezi oktoba 2014 ambapo kampuni ya coca cola ilisaini mkatabawa udhamini na
klabu yetu. Kampuni ya Coca Cola itakuwa inatoa fedha taslimu Tsh 60 milioni
ambazo inazitoa kwa mwaka. Fedha hizi hutolewa kila baada ya robo mwaka
shilingi milioni 15. Hii ina maana kuwa coca cola inatoa shilingi 5,000,000.00
milioni kila mwezi.
Hivyo
kuanzia mwezi oktoba klabu inapata toka kwa wadhamini wake wawili (Binslum Tyre
Co Ltd na Coca Cola Kwanza) shilingi 20,000,000.00 kwa mwezi. Fedha hizi
zinachangia asilimia 40.8(%) ya gharama za uendeshaji wa timu kwa mwezi na
asilimia 59.2(%) ya gharama hizo bado zinabebwa na Halmashauri.
Uwepo
wa wadhamini hivi sasa haujaongeza fedha kutoka katika bajeti hiyo bali
umepunguza utegemezi wa timu kwa Halmashauri.
Hivyo
basi shutuma zinazotolewa na baadhi ya wadau kuwa changamoto ambazo timu
inazipitia kwa sasa ni kutokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini ni UPOTOSHAJI
MKUBWA.
MWISHO
Post a Comment