Majirani wakilia kwa uchungu |
Mke wa Marehemu akiwa chini baada ya kushudia mwli wa marehemu mumewe ambaye ameachwa na watoto watatu.. |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida Mkazi wa eneo la Mama John Mtaa wa Kagera jijini Mbeya ambaye jina lake
halijafahamika mara moja maarufu (Malebo) Dereva wa Daladala (34) amekutwa amejinyonga
hadi kufa ndani ya nyumba ya mpenzi wake (Mchepuko) Octoba 31 mwaka huu .
Tukio hilo la aina yake
limetokea majira ya saa 7 jioni katika eneo la Mama John jijini hapa ambapo
inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi kwani marehemu huyo ilikwenda kwa mpenzi wake (Mchepuko)na kukuta nyumba ikiwa wazi bila kuwa na dalili za kuwa
na mtu ambapo mara baada ya kuuliza majira alielezwa kuwa mwanamke huyo
hakuonekana nyumbani hapo kwa usiku mzima nakwamba hakulala kwakwe.
Aidha baada ya kupata majibu
hayo mwanaume huyo aliondoka na kwenda kwa marafiki zake sehemu wanayouzia
pombe za kienyeji maarufu (Vamponji)
na kuomba ushauri juu ya nini afanye ili kukabiliana na hali hiyo.
Alidaiwa kuwa mwanaume huyo
wakati akiomba ushauri alieleza kuwa mpenzi wake huyo ambaye alijulikana kwa
majina ya Rebeka Dankeli maarufu Mama Chausiku alihisi amekwenda kulala kwa mwanaume mwingine
kwani wamekuwa wakigombana kw amuda mrefu juu ya kuwepo kwa hali hiyo.
Wakati akitoa malalamiko
hayo kwa marafiki zake alielezwa kuwa nivema mambo hayo wakayamaliza wenyewe kwani
imekuwa kero kwao hasa kutokana na kwamba wamekuwa wakigombana mara kwa mara na
kushulishwa na majirani hao hivyo wamechoka na kwamba aondoke na akayamalize
yeye mwenyewe.
Kutokana na hali hiyo
mwanaume huyo aliondoka katika eneo hilo la kuuzia pombe za kienyeji iliopokwenda
kupata ushauri na kurudi katika nyumba anapoishi hawala yake huyo huku
akiendelea kutafakari yale yanayomsibu katika moyo wake pamoja na kuangalia
kama mwanamke huyo atarudi au laa.
Baada ya kukaa kwa muda
mrefu pasipo kumona mpenzi wake ambapo ilikuwa imefika majira ya saa mbili
kasoro aliamua kuchukua maamuzi ya kukatisha uhai wake kwa kujinyonga.
Akizungumzia hali hiyo
Mwenyekiti wa Mtaa huo Ndugu Anyokisye
Mwambona amesema tukio hilo la kujinyonga kwa mwanaume huyo nilakwanza kutokea
katika maeneo hayo.
Amesema taarifa za
kujinyonga alizipata majira ya saa mbili kasoro ambapo alichukua jukumu la
kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa lengo kutoa mwili wa marehemu huyo ndani
ya nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti
huyo anasema mwanaume huyo tayari alikuwa na mke wake na alikuwa na watoto
watatu hivyo tukio hilo limetokea kwa nyumba ndogo (Mchepuko) nakwamba kesi juu ya mwanaume huyo amekuwa akizipata
mara kwa mara hivyo hatua ya mwanaume
huyo kujinyonga inawezekana ikawa ni wivu wa mapenzi.
Amesema tuko hilo liliteka hisia za wakazi
wengi wa eneo hiloo kwani mwanaume huyo alikuwa na familia yake hivyo maamuzi
aliyoyachukua ni makubwa na yataigharimu familia yake kwa kiasi kikubwa hasa
kutokana na watoto wenye kuwa na umri mdogo pamoja na mke wake kutokuwa na
shughuli yoyote.
Vilio na majonzi yalitawala
baada ya mke wa marehemu huyo halali alipofika katika eneo hilo la tukio na
kuanza kulia kwa sauti kubwa huku akitamka maneno ambayo yaliwaliza wengi
walitokea katika tukio hilo.
Alidai kuwa amekuwa
akimkanya mumewe huyo kwa muda mrfu juu ya kuachana na mwanamke huyo lakini
amekuwa hasikii hivyo yaliyokumkuta ni ukaidi wake alieleza mama huyo huku
akitazama mwili wa mumewe ukuwa juu uneninginia .
Hata hiyo Kamanda wa polisi
Mkoani hapa Ndugu Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya rufaa mbeya.
Mwisho.
Post a Comment