| Meneja wa TRA Mbeya Anord Maimu akizungumza na waandishi wa habari juu ya kaunza kwa maadhimisho ya siu ya Mlipa kodi inayotalajiwa kaunza Nov 17 hadi 21 mwaka huu. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
MAMLAKA
ya Mapato TRA Mkoa Mbeya imewataka wafanyabiashara kutambua kuwa suala la
matumizi ya mashine za EFD lipo kisheria hivyo ni vema wakaitekeleza kuliko
kuendelea kutupiana lawama.
Imesema,
bunge ndio lililopitisha sheria hiyo na mamlaka inawajibika katika
usimamizi na utoaji wa elimu hivyo hakuna haja ya kuendelea na mvutano.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja wa mamlaka ya
Mapato Mkoa wa Mbeya, Anord Maimu, wakati akizungumza na waandishi juu ya
kuadhimisha wiki ya mlipa kodi ambayo kila mwaa huadhimishwa na mamla hiyo.
Amesema,
mamlaka haitungi sheria kwani sheria zote wanazozisimamia zimepitishwa na Bunge
hivyo suala la mashine lililipitishwa na bungeni na wenye wajibu wa
kulitekeleza ni TRA.
Amesema,
kazi kubwainayofanywa na TRA ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya matumizi
ya mashine hizo pamoja na umuhimu wake katika kuinua pato la Taifa kupitia mashine
hizo.
Amesema
wao kama mamlaka hawana mvutao wowote na wafanyabiashara hao kama ambavyo
imekuwa ikitafsiliwa na wengi badala yake wao wamekuwa mstari wa mbele katika
kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya mashine hizo.
Aidha,
Maimu aliwataka wafanyabiashara hao kuitumia vizuri siku ya mlipa kodi
inayotarajia kuanza November 17 mwaka huu na kilele chake kufanyika November 21
katika ukumbi wa Mkapa.
Hata
hivyo, alisema katika siku hiyo TRA inakusudia kufanya shughuli mbalimbali
zilizoambatana na utoaji huduma kwa makundi muhimu ya jamii kama vile utoaji wa
vyandarua 50 na shuka 50 katika hospitali ya Wilaya ya Kyela.
Mwisho.






Post a Comment