Mswada
uliopitishwa na bunge la Gujarati siku ya jumatatu pia unataka viongozi
waliochaguliwa kubaini katika kipindi cha miezi sita iwapo wana vyoo nyumbani
la sivyo waondolewe katika nyadhfa zao.
''Kukabiliana
na watu wanaokwenda haja katika maeneo ya wazi ni muhimu kwa lengo la
kuimarisha mazingira safi mbali na uchafuzi wa maji','ilisema serikali.
Gujarat
ni jimbo la nyumbani la waziri mkuu mpya Narendra Modi ambaye amesema kuwa kila
nyumba ni sharti imiliki choo katika kipindi cha miaka minne ili kuzuia
magonjwa yanayosababishwa na watu kwenda haja katika maeneo ya wazi.
Mamilioni ya raia
nchini India hawana vyoo.
Hatahivyo
raia hao wanadaiwa kuwa na tatizo la utumizi wa vyoo.hii ni kwa sababu kila
sekunde mtu mmoja huenda haja katika eneo la wazi,swala linalosababisha ugonjwa
wa utapia mlo miongoni mwa watoto, kushuka kwa uchumi pamoja na ghasia dhidi ya
wanawake.
Ni
tatizo ambalo waziri mkuu Narendra Modi ameamua kuhakikisha kuwa kila nyumba
ina choo ifikiapo mwaka 2019.
Lakini
kulingana na wataalam wa usafi ,jibu halitapatikana iwapo kutajengwa vyoo zaidi
vya kuogea ,kwanza raia ni sharti waanze kupendelea kwenda katika vyoo.BBC SWAHILI







Post a Comment