Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Na Boniface Wambura,Dar es salaam
Usajili wa dirisho dogo msimu wa 2014/2015 umefungwa jana (Desemba 15 mwaka huu) huku wachezaji 15 kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka nchi mbalimbali.

Wachezaji walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam, Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.

Dan Serunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murushid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.

Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Serunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo.

Wakati huo huo  Michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 ngazi ya Taifa inaendelea leo jioni (Desemba 16 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani.

Uwanja wa Nyumbu uliopo mkoani Pwani utazikutanisha timu za Mjini Magharibi na Dodoma katika mechi ya kundi B, wakati kundi C kutakuwa na mechi kati ya Arusha na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Wakati kesho (Desemba 17 mwaka huu) ikiwa ni mapumziko, michuano hiyo itaingia hatua ya robo fainali keshokutwa (Desemba 18 mwaka huu) kwenye viwanja hivyo hivyo.
 Mwisho

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top