Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari la polisi tayari kupelekwa kuhifadhiwa katika hospital ya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara
moja amekutwa amekufa na mwili wake ukiwa ndani ya shimo la choo ambalo
lilikuwa halitumiki.
Tukio hilo limetokea leo Des26 saa 6 mchana mwaka huu katika
kijiji cha Mgongani Wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo kwa mujibu wa mashuhuda
wa tukio hilo wamedai kuwa mama huyo ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi 8
inadaiwa alipigwa na mumewe kisha mwili wake kutumbukizwa ndani ya shimo la
choo.
Wamedai kuwa mwanaume huyo mara baada ya kutekeleza mauji hayo
aliutumbukiza mwili huo ndani ya shimo
hilo la choo kisha kutokomea pasipo julikana mwili wa mama huyo umehifadhiwa
katika hospital ya wilaya ya Bunda Mkoani Mara..JAMIIMOJABLOG
|
Post a Comment