Katika hali isiyokuwa ya
kawaida Mkazi wa kijiji cha Nyamongo Tarime Mkoani Mara ambaye jina lake
halikufamika mara moja amemkata mguu mmoja ng'ombe baada ya
kuvamia shamba lake na kula mazao shambani hapo.
Tukio hilo la aina yake limetokea juzi Mkoani Mara katika kijiji hicho
cha Nyamongo ambapo ng'ombe huyo alikutwa na mmiliki wa shamba na kupewa adhabu
hiyo.
Tukio hilo la iina yake
limestaajabisha wengi huku ikidaiwa kuwa huenda vitendo hivyo vinafanyika
kutokana na viongozi husika kushindwa kutatua migogoro ya namna kat ya wafugaji
na wakulima katika mkoa huo.
Wakizungumza kwa mshangao mkubwa watu walio shuhudia tukio wamesema kuwa
ukatili huo haupaswi kuungwa mkono kwani huenda ukaleta madhara makubwa katika
jamii hiyo.
Aidha mguu wa ng'ombe wa upande wa kushoto umeendelea kuimalika majeraha huku maisha yakiendelea kama kawaida.
mwisho.
|
Post a Comment