Kaimu Katibu tawala wilaya ya Mbeya bi. Quip Mbeyela ambaye alimuwakilisha mkuu wa wilaya mbeya
Kampuni ya Serengeti breweries Mkoani Mbeya (SBL)imetoa Rai kwa wazazi na walezi wasio na uwezo wa kuwasomesha watoto wao elimu ya juu kupeleka maombi ili waweze kupata udhamini kutoka katika kampuni hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa uhusiano wa kampuni hiyo bw. Evance Mlelwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ghala mpya ya kuhifadhia vinywaji vinavyo zalishwa na kampuni hiyo.
Mlelwa amesema kuwa kampuni hiyo inatoa ufadhili wa asilimia miamoja (100) na kwamba hadi sasa kampuni ya serengeti breweries imewafadhili wanafunzi zaidi ya 30.
Kuhusiana na ujenzi huo wa ghala Mlelwa amesema ujenzi huo umeghalimu sh.500milioni ambapo ghala hilo limejengwa katika eneo la Iyunga jijini hapa.
Aidha kwa upande wake Kaimu Katibu tawala wilaya ya Mbeya bi. Quip Mbeyela ambaye alimuwakilisha mkuu wa wilaya mbeya amesema serikali bado inatambua mchango mkubwa unaotolewa na kampuni hiyo hususani katika suala la ajira.
Amesema kwa kiwango kikubwa sekta binafsi ndio imekuwa mchango mkubwa kwa serikali katika suala la ajira hivyo hatua hiyo inastahili pongezi kwani imeongeza fursa za ajira kwa wakazi wa eneo hilo na jiji la mbeya kwa ujumla.
|
Post a Comment