Wakati raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inakamilika leo
(Desemba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu, ligi hiyo itaingia raundi ya tisa
Januari 3 mwakani kwa mechi tano.
Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika
Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex,
Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati
Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ligi hiyo ambayo itachezwa mfululizo
(non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani, itakamilisha raundi ya tisa
Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba kwenye Uwanja wa
Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda kwenye Uwanja wa
Sokoine.
Nayo mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand
United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika ya 6 imemaliziwa leo ambapo timu
hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Wakati huo huo, mechi ya ligi iliyochezwa
jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi
cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Hamisi Kasanga.
MWISHO
Post a Comment