Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wa pili kulia pamoja na viongozi wengine wa mkoa wakitazama mchezo wa amani kati ya Viongozi waMadhehebu ya  Dini na viongozi wa serikali katika uwanja wa Sokoine jijini mbeya Des9 mwaka huu katika maadhimisho ya sherehe za Miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mshambuliaji wa Timu ya Viongozi wa serikali Profesa Norman Sigalla Mkuu wa (Wilaya ya Mbeya)  akijaribu kuwapita mabeki wa Timu ya Viongozi wa Dini ambapo katika mchezo huo Viongozi wa Dini waliibuka kidedea kwa ushindi wa goli 4 kwa mbili katika mchezo huo huku Profesa Sigalla akiwa kivutio kutokana na umahili wake wa kukaba na kutoa pasi.








Kikosi cha Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoani Mbeya
Kipa wa Viongozi wa Serikali Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi akitoka nje ya uwanja mara baada ya kupata majeraha katika mchezo huo wenye lengo la kudumisha amani katika mkoa huo.Picha na (David Nyembe Fahari News)


Kikosi cha Viongozi wa serikali 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akitoa neno kwa washiriki wa mchezo huo ambao ni Viongozi wa dini katika madhehebu yote Mkoani humo pamoja na Viongozi wa serikali.




Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top