Afisa elimu wa Mkoa wa Mbeya, Remigius Ntyama
Na Emanuel Madafa
JUMLA
ya wanafunzi , 28,780 waliomaliza elimu yao ya msingi mwaka 2014 katika Mkoa wa
Mbeya,wamechaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari January
,2015.
Akitoa
taarifa hiyo jana, Afisa elimu wa Mkoa wa Mbeya, Remigius Ntyama, alisema idadi
hiyo ni sawa na asilimia 98.55 licha ya kukabiliwa na changamoto
kubwa ya kutofikia Malengo ya Matokeo Makubwa Sasa(BRN).
Alisema,
wanafunzi waliochaguliwa katika shule za bweni ni 255
kati yao wavulana 168 na wasichana 87 sawa na asilimia o.89.
Alisema,
wanafunzi 28,365 kati yao wavulana ni 13,861 na wasichana 14,504 wamechaguliwa
kujiunga katika shule za kutwa.
Aidha,alisema
kuwa wasichana 160 sawa na asilimia 0.6 kutoka halmashauri ya Busokelo, Ileje,
Kyela na Rungwe wamechaguliwa kujiunga na shule ya wasichana ya Kayuki iliyopo
Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Akizungumzia kushuka
kwa kiwango cha ufaulu, Ntyama alisema kuwa kwa miaka mitatu mfululizo, ufaulu
wa wanafunzi Kimkoa umekuwa ukipanda lakini mwaka 2014 ufaulu
umepanda kwa kiasi kidogo kwa asilimia tatu japo yapo chini ya asilimia 60
ambayo ni malengo ya BRN.
Alisema,hali
ya kutofikiwa malengo kwa mkoa wa Mbeya ni changamoto kubwa ambayo kwa pamoja
viongozi na jamii inatakiwa kutambua kuwa tumepatwa na janga ambalo
kila mmoja wetu anatakiwa awajibike.
Hata
hivyo, alitoa wito kwa viongozi wote wa serikali, wadau wa elimu wote kwa
ujumla kuweka mikakati ya dhati katika kusimamaia, kutekeleza na kutoa maamuzi
sahihi katika kuboresha elimu ndani ya Mkoa wa Mbeya.
Mwisho.
|
Post a Comment