Katika
kutambua mchango unaolewa na viongozi wa serikali ndani ya jamii viiongozi wa
madhehebu ya dini Mkoa wa Mbeya, wamemtunuku cheti bora cha
utumishi, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Norman Sigalla baada ya kuridhika na
utendaji kazi wake ulioambatana na uwajibikaji mzuri kwa wananchi.
Akizungumza
na akizungumza jijini Mbeya , Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Calvary
Tabernacle Church Kael Mwaisumo, alisema kiongozi huyo anastahili
kutunukiwa cheti hicho cha utumishi bora kwa kuweza kukidhi vigezo na sifa za
uongozi uliotukuka ndani ya jamii anayoiongoza.
Amesema,
baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa
wananchi na watendaji wa chini jambo ambalo amelipinga kufanywa na kiongozi
huyo ambaye ameonekana kuwa mstali wa mbela katika kutatua migogoro ya kijamii
husasani ya kidini.
Aidha,
akizungumzia tukio hilo, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mohamedy Mwansasu, ametumia
nafasi hiyo kummwagia sifa kiongozi huyo kwa kuhubiri suala la
uadilifu na uwajibikaji kwa watu anaowaongaza hali iliyosaidia kupatikana kwa
amani kwa Mkoa wa Mbeya ambao umekuwa na historia ya kuibuka kwa vurugu za mara
kwa mara.
Amesema,
viongozi wa serikali wanapaswa kuwa na sifa za
uwajibikaji huku wakitambua na kuthamini masuala makubwa
ya kiutendaji wanayoyafanya kwenye jamii husika.
Hata
hivyo, amesema kuwa endapo viongozi wa serikali watatambua kwamba uongozi ni
dhahama, wataweza kupunguza kwa asilimia kubwa manung’uniko yanayotolewa na
wananchi.
Mwisho.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Profesa Norman Sigalla akizungumza na viongozi hao wa madhehebu ya dini ofisni kwakwe baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo. |
Maombi |
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mohamed Mwansasu akizungumza katika hafla hiyo.Picha na David Nyembe wa Fahari News. |
Post a Comment