Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anatarajiwa kuhutubia maelfu ya wajumbe katika siku ya mwisho ya mkutano mkuu wa chama tawala cha ZANU-PF mjini Harare.
Katika hotuba yake Bwana Mugabe anatarajiwa kutangaza nani atachukua nafasi ya makamo wa rais, Joice Mujuru, ambaye ametuhumiwa kufanya ufisadi.
Waandishi wa habari wanasema aliyeelekea kuteuliwa ni waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa, lakini baadhi ya watu wanasema Rais Mugabe huenda akamteua mkewe, Grace, kuwa naibu wake.
Makamo wa rais ndiye huenda akarithi uongozi kutoka kwa Bwana Mugabe ambaye ametimia miaka 90.CHANZO BBC

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top