| Omar Sheriff alidai kuwa na nguvu za kimiujiza za kuwaponya wanawake kwa kuwatoa mashetani kutoka sehemu zao za siri
Muhubiri wa zamani aliyedai kuwa na 'nguvu za kuponya' amepewa
adhabu ya kifungo cha nje cha miaka ishiriki kwa kumyanyasa kimapenzi mwanamke
mmoja nchini Australia.
Muhubiri
huyo alidai kutumia kile alichokiita 'nguvu za kipekee' za uponyaji
kumdhalilisha kimapenzi mwanamke huyo akisema kuwa alikuwa na mashetani katika
sehemu yake ya siri.
Omar
Sheriff, mwenye umri wa miaka 67, alimwambia mwanamke huyo mnamo mwaka 1994
kwamba alikuwa na mashetani mwilini mwake na kwamba mashetani hayo yalipaswa
kuondolewa kwa njia maalum katika kiwanda chake cha fanicha mtaani
Campbellfield.
Kwa
mujibu wa taarifa za jarida la 'The Age', jaji Jane Patrick alifahamishwa kuwa
Omar alidai alikuwa na nguvu kubwa sana za kimiujiza na alimuonya mwanamke huyo
aliyekuwa na miaka 30 kwamba angefariki ikiwa mashtenai hayo hayangetolewa
kutoka katika sehemu yake ya siri.
Alisema
alikuwa na utabiri kuhusu maisha yake na kumwambia kuwa angepata shida kubwa
sana ikiwa asingetolewa mashteni hayo.
Sheriff
aliwahi kufungwa jela mwaka 1997 kwa miaka minane lakini adhabu yake
ilipunguzwa hadi miaka sita kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu kwa madai hayo
hayo.
Shariff
hakumbaka tu mwanamke huyo bali wanawake wengine watatu.
Jaji
alimwambia Sheriff kwamba wanawake hao waliokuja kwake na matatizo ya kindoa
walimwamini sana kwamba angewasaidia lakini wao ndio walikuwa waathiriwa wa
kwanza wa upuzi wa ''nguvu zake za kimiujiza''
Sheriff
alikiri makosa matatu ya kuwaingilia kimwili wanawake kwa kuwahadaa, makosa
aliyoyafanya kati ya Januari na Disemba mwaka 1994.
Mahakama
iliambiwa kuwa baada ya muhubiri huyo kuwabaka wanawake hao aliwaambia waje na
chupa ya Coca-Cola, mayani na ubavu wa nyama ya Kondoo.
Alikuwa
anawaingiza ndani ya nyumba yake na kuwapeleka katika chumba chake ambako
aliwatendea unyama huo mara kwa mara.
Katika
hukumu yake Jaji Patrick alisema kuwa Sheriff, anakabiliwa na matatizo ya
kiafya na changamoto za kisaikolojia na kwamba kwa sababu alikiri makosa basi
ameoneolea waathiriwa wake uchungu wa kuanza kutoa ushahidi.CHANZO BBC
|
Post a Comment