Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Profesa Norman Sigalla akizungumza na wajasilimali wa Mkoa wa Mbeya katika semina iliyoandaliwa na Benki ya Posta (TPB)Tanzania katika ukumbi wa Mikutano Mtenda. |
Wajasilimali wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
SERIKALI Mkoani Mbeya imezitaka Taasisi za kifedha (Mabenki) kuhakikisha wanaanzisha kitengo maalumu cha kuwawezesha wafanyabiashara kutambua aina gani ya miradi wanatakiwa kuanzisha ili kuwalahisishia kupata mikopo katika taasisi hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo
jijini Mbeya na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Profesa Norman Sigalla wakati
akizindua mafunzo kwa wajasilimali yaliyoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania yaliyofanyika
katika ukumbi wa Mtenda ambapo wafanyabiashara waliopota fursa ya kuhudhuria
semina hiyo ni zaidi ya 150.
Amesema kumekuwepo na changamoto
kubwa kwa wafanyabiashara juu uanzishwaji miradi ya biashara hivyo umefika
wakati kwa taasisi hizo kuanzisha dawati maalumu litakalo husika moja kwamoja
na kusaidia wafanyabiashara hao katika eneo la maandiko ya miradi.
Amesema
kuwepo kwa kitengo hicho pia kutasaidia kuepusha
wateja wao kurubuniwa na watu wan je ambao wamekuwa wakiwashauri tofauti na
malengo ya mkopo.
Amesema baadhi ya wafanyabiashara
wamekuwa wakikwama katika kutimiza malengo yao ya kibiashara kutokana na
udanganyifu wa maandiko ya shughuli anayokusudia kuifanya hivyo suala hilo
litaondoa migongano hiyo.
Aidha amesema,ni vema andiko mradi likaenda
sambamba na uhalisia wa shughuli ya kibiashara inayokusudiwa kufanywana
mlengwa, ambayo pia itakuwa imekidhi viwango vya ubora utakaoendana na
ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Posta, Sabasaba Mushingi, alisema lengo la
benki hiyo kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali zaidi ya 150
katika Mkoa wa Mbeya ni kuwawezesha kujua umuhimu wa huduma za kibenki hususani
mikopo.
Amesema Benki hiyo ya
posta imejitahidi kwa kiwngo kikubwa katika kupunguza suala la ukubwa wa viwango vya riba
vinavyotolewa na mabenki nchini,ambapo kwa benki ya hiyo ndiyo imeweza
kuwa na riba ndogo kuliko mabenki mengine kwa hapa nchini.
Mwisho.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Posta, Sabasaba Mushingi, |
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja n wafanyakazi wa benki ya posta Tanzania Mkoa wa Mbeya |
Post a Comment