Na Emanuel Madafa,Mbeya
Sakata la kuvunjiwa mkataba
mchezaji , beki wa clabu ya Mbeya City, Deogratus Julius, limeendelea kuchukua
suala mpya ambapo mchezaji huyo ameibuka na kudai kuwa yeye hana ungomvi na
uongozi wa klabu hiyo licha ya kumsitishia mkataba wake badala yake ameutaka
uongozi huo kumlipa haki zake za msingi pamoja na mishahara mitatu ambayo
hakulipwa.
Akizungumza na blog hii Deogratus, amesema kuwa clabu hiyo
inahaki ya kutekeleza na kufanya kile wanachoona kinafaa lakini yeye
anachokihitaji ni kulipwa haki zake za msingi na kamwe hawezi kujutia maamuzi
yake kwani timu hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa majungu, chuki na fitina.
Amesema, hayuko tayari kuichezea
timu hiyo kwani walichomfanyia ni zaidi ya unyama, hivyo anachokihitaji yeye ni
kulipwa haki zake za msingi kama sheria na taratibu za mkataba zinavyoelekeza.
Amesema, moja ya sababu ambazo
zimeelezwa kwenye barua hiyo ni kwamba yeye ameonekana kuwa kinara wa
kushawishi migomo, kupigana na wenzie jambo ambalo si kweli kwani hata baadhi
ya wachezaji wenzake wameoneshwa kushangazwa na tuhuma hizo zilizoelezwa na
uongozi huo.
Amesema, maamuzi hayo yameweka
bayana kwamba kuna agenda ya siri iliyokuwa imejificha ndani ya klabu hiyo
kwani mchezaji anapokosea huitwa na kuhojiwa kama jambo
linalosemekana kulifanya linaukweli au la lakini cha kushangazwa ni uongozi
huo kufanya maamuzi bila ya kumtendea haki mtuhumiwa kitendo ambacho ni kinyume
cha sheria na utaratibu.
Aidha, Deogratusi akielezea sababu
ya kudai kuwa timu hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa majungu, hila na visasi,
alisema kuwa wachezaji wote ambao wameonekana kuwa ni zao kutoka kwa aliyekuwa
kocha msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalwisyi, wameonekana kuundiwa zengwe la
kuondolewa.
Akizungumzia kuhusu maamuzi hayo
kufanyika kwa hila na chuki, mchezaji huyo amesema kuwa kama viongozi hao
walikuwa na utu na busara wasingesubili kufungwa kwa usajili wa dirisha dogo,
wangefanya uungwana wa kumpa nafasi ya yeye kuangalia mstakabari wa
maisha yake kwa kuingia mikataba na timu nyingine.
“Kitendo hiki ndio kilichonifanya
ni tambue kuwa viongozi hawa wamelifanya jambo hili kwa kunikomoa
kwani nimeudhuria mazoezi yote, lakini ninacho kifanya mimi ni
kumshukuru mungu kwa kila jambo, na nitaendelea na mazoezi yangu kwa
kusubili msimu ujao wa ligi ila uongozi naomba unitendee haki kwa kunipa haki
zangu,”alisema.
Aliyekuwa beki wa clabu ya Mbeya City, Deogratus Julius, |
Naye Katibu wa Clabu ya Mbeya City,
Emmanuel Kimbe, akizungumzia sakata hilo, amesema kuwa wachezaji wote
wanafahamu sheria na taratibu za timu hasa kwenye suala zima la nidhamu hivyo,
mchezaji huyo ameonekana kuwa kinara wa utovu wa nidhamu na uongozi umeamua
kuvunja mkataba .
Akieleza sababu za uongozi kumkabidhi
barua mchezaji huyo mara tu ya kufungwa kwa usajili wa dirisha dogo, Kimbe
alisema, ni kweli barua hiyo ilichapwa Desember Mosi lakini haikuwa
rahisi kumkabidhi mchezaji huyo kwani kipindi hicho wachezaji walikuwa
mapumziko na hata walipoingia kambini yeye alifika kwa kuchelewa.
Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo
ambao waliomba kuhifadhiwa majina yao, wakizungumzia hilo, walisema
kuwa wamoonyeshwa kushangazwa na kuingiwa hofu na uongozi huo, kwani wanakiri
kwamba mchezaji mwenzao huyo hajawahi kuhusika na tuhuma hizo na kwamba ndio
kwanza wanazisikia.
“Nina mfahamu Deogratus ndani na
nje lakini ndio kwanza nayasikia haya unayoniuliza lakini ndugu yangu Mwandishi
kunamambo mengi yanayoendelea ndani ya timu hii kwani wapo baadhi ya wachezaji
ambao walihusika na utomvu wa nidhamu wa kutoroka kambini na kwenda kulala na
wanawake zao majumbani lakini hawajachukuliwa hatua,”alisema mmoja
wa wachezaji hao.
Hata hivyo, akizungumzia hilo,
Mwalimu wa klabu hiyo, Jumba Mwambusi kwa njia ya simu, alisema yeye si msemaji
na kwamba endapo waandishi wanahitaji ufafanuzi wa suala hilo aonane na utawala.
Kwa upande wao mashabiki wa klabu
hiyo, wamelaani kitendo hicho kilichofanywa na uongozi wa klabu hiyo kwamba si
cha ubinadamu kwani wakumbuke mpira ni kazi hivyo hiyo ilikuwa ni ajira ya mchezaji
huyo ambaye pia alikuwa akitegemewa na ndugu na familia yake.
Wamesema maamuzi yaliyofanywa na uongozi wa klabu hiyo
haupaswi kuungwa mkono na mtu wa aina yeytoe kwani tafsiri ya neon mpira
limegeuzwa kuwa sehemu ya chuki na ugomvi hali ambayo si njema katika maendeleo
ya soka hapa nchini.
Mwisho.
Mwisho.
Post a Comment