Kaimu afisa wa Idara ya Forodha, Majaliwa Omary akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Tunduma |
Bidhaa zilizokamatwa katika baadhi ya Bar Mjini Tunduma ambazo zimeingia nchini kinyume cha taratibu kupitia njia za Panya. |
Afisa ukaguzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Yusto Wallace |
Hii ni halali kwa soko la Tanzania ambayo ina nembo ya Mabibo Beer kutoka Namibia |
Hii si halali kwa soko la Tanzania ikiingizwa nchini kupitia njia za Panya ikitoke nchini Sauth Afrika |
Na EmanuelMadafa,Tunduma
Kwa kiwango kikubwa serikali
imekuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha
kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya njia za panya zinazotumiwa na
baadhi ya wafanyabiashara kwa kupitishia
bidhaa za magendo katika maeneo ya mipakani.
Hali
hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa
wakitekeleza sheria za ulipaji wa kodi, kushindwa kuendesha biashara hizo
kutokana na uwepo wa bidhaa zinazoingizwa kwa njia ya magendo sokoni.
Akizungumza
na waandishi wa habaari, Meneja biashara wa kinywaji cha Bear aina ya , Wind hock Ndugu Joseph
Boniface, amesema serikali inatakiwa kudhibiti njia zote za panya ambazo
zinatumiwa na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa zao kwa njia ya magendo ili
kutenda haki kwa wale wanaochangia pato la taifa kwa kulipa kodi.
Amesema
kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo serikali bado itaendelea kupoteza kiasi
kukubwa cha fedha pamoja na kuongeza bidhaa ambazo ubora wake haukidhi soko la
ndani.
Amebainisha kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo katika mji huo wa tunduma hususani kwa baadhi ya bar na hotel zimekuwa zikuza bidhaa hiyo ya Bear ya Wind hock ambayo imeingizwa nchini kinyume cha sheria ikitokea Afrika ya Kusini na kuingia Tanzania kwa njia ya panya kwa kupitia mpaka wa Tunduma.
Akizungumzia
changamoto hiyo Kaimu afisa wa
Idara ya Forodha, Majaliwa Omary alisemaa ni ngumu
kudhibiti magendo kutokana na hali ya uwazi na njia za panya
zilizokithiri ndani ya mpaka huo.
Amesema, kutokana
na mianya hiyo magari yamekuwa yakipitisha bidhaa halamu na halali kwa kutumia
njia za panya na kuingia upande wa pili wa mpaka ama kuingiza nchini pasipo
vikwazo hali ambayo imechangia pia udhibiti mdogo wa bidhaa kama dawa, vyakula
na vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku.
Naye
Afisa ukaguzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Yusto
Wallace, aliitaka jamii kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa ambazo zimekaguliwa
na mamlaka za udhibiti.
Aidha,aliiomba
serikali kuijengea uwezo TFDA hasa katika kuajiri watumishi wanaokidhi mahitaji
ya udhibiti ili kukabiliana na ongezeko kubwa la wafanyabiashara ambao
wanaendesha shughuli zao kinyume cha utaratibu.
Hata
hivyo,amesema TFDA imeweza kukamata shehena ya vinywaji mbalimba ambavyo
vimeingizwa nchini kinyume cha utaratibu na zilizomaliza muda wake wa kutumika
ikiwemo Bear aina ya Wind Hock ya kutoka Afrika ya Kusini.JAMIIMOJABLOG
Mwisho.
Post a Comment