Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
Na EmanuelMadafa
WATU 9 wamepoteza maisha  papo hapo na wengine 13 kujeruhiwa mkoani Mbeya baada ya basi ndogo ya abiria aina ya Coaster  lenye namba za usajili T 203 ARZ kuyagonga magari mawili.

Akizungumzablog hii Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi aliyekuwa katika eneo la tukio, amesema  tukio hilo lilitokea  majira ya saa nane za mchana katika eneo la Sengula  Kata ya Tunduma Wilayani Momba.


Amewataja waliofariki katika ajali ya Tunduma kuwa ni Amina Michael,Neema Almasi, Rose Hezron Halele, wakazi wa Tunduma, Hebeli Mkilimi Mkazi wa Ileje, Thomasi Simfukwe mkazi wa Hamwelo Mbozi, Exavery Mubiso mkazi wa Ukwile Mbozi na watu wengine watatu hawajatambulika ambao walipata ajali katika eneo la Sogea Tunduma na Hamad Imani Masawe mkazi wa Dar Es salaam na kwamba wote ni watu wazima.


Amesema majeruhi katika ajali ya Sogea Tunduma walikuwa 24 ,12 kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao, wane wamelazwa hospitalini hapo na 12 wamekimbizwa hospitali ya rufaa kwa matibabu zaidi.

Amewataja waliolazwa kuwa ni Vicky Michael Ngowi (33), Grace Mgimba (33), Sharifa Jemadari(25), Christina Mtende(31), Zainab Jamadin (1), wote wakazi wa Tunduma, Eneth Mkomanga(17) mkazi wa Ilembo ambao wamepelekwa hospitali ya Rufaa Mbeya.

Wengine ni Jackson Mwashambwa mkazi wa Mlangali, Cyprian Mwananzumi (50) mkazi wa Njombe, Siamini Sichenje(30) Emmanuel kamwela(9)mkazi wa Tunduma, na John Zumba mkazi wa Mlowo.

Kamanda, Msangi alisema kuwa Coaster hiyo ikiwa inaendeshwa na dereva asiyefahamika ilikuwa likitokea Mbeya kwenda Tunduma hivyo kukutana na maswahiba hayo wakati likijaribu kulipita Lory la mizigo aina ya Tata lenye namba za usajili T 789 AZL lililokuwa mbele yake.

Alisema, Coaster hiyo ikiwa inapandisha kilima kidogo kilichopo kwenye eneo hilo na kujaribu kulipita Lory, mbele yake lilitokea basi kubwa la abiria ambalo lilikuwa likitokea Sumbawanga kuelekea Mbeya, hivyo dereva wa Coaster kushindwa pa kukimbilia na kuhamua kulipenyeza gari hilo katikati ya magari hayo mawili.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi, inadaiwa kwamba Coaster hiyo ilienda kuligonga Lory la mizigo upande wa kulia na upande wa kushoto kuliparamia basi kubwa na kusababisha vifo vya watu  sita na kujeruhi 13.

Aidha, alisema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya serikali ya Tunduma na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi na Tunduma.
.
Mwish


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top