Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This




Mkuu wa shule hiyo ya Mbozi yenye kidato cha kwanza hadi sita,  Eliya Msyaliha, akionyesha baadhi ya vifaa vilivyo tolea na wafadhiri hao.




Mwalimu wa masomo ya Sayansi katika shule hiyo Sijali Mpesya akiwa na wanafunzi wake 



Na Mwandishi wetu,Mbozi.
Umoja wa Wakristo wa kanisa la Muhlaker lililopo katika mji wa Wurttemburg, nchini Ujeruman limetoa msaada wa vifaa  mbalimbali vya masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari ya Mbozi, vyenye thamani ya mamilioni ya fedha.

Kadhalika, shule hiyo, mbali na kupewa vitabu vya masomo yote yaliyo kwenye mkondo wa sayansi, pamoja na vifaa mbalimbali vya kisasa vya maabara, pia imepokea msaada wa fedha kiasi cha sh.mil 11.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa shule hiyo ya Mbozi yenye kidato cha kwanza hadi sita,  Eliya Msyaliha,  alisema vifaa hivyo vimetolewa  kwa nyakati tofauti kupitia program ya ushirikiano kati ya wafadhili hao na shule.


Amesema shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania kusini M agharibi kwa muda mrefu limekuwa na utaratibu wa kushirikiana na wakristo hao wa nchini Ujerumani.


Ameongeza kuwa mbali na vifaa, lakini pia kumekuwa na program mahususi ya wakristo wan chi hiyo na washirika wao kutoa msaada wa walimu wa masomo ya sayansi, ambao mara kadhaa huja kufanya kazi shuleni hapo.

Aidha, amesema kuwa wafadhili wengine wa Mission 21 wa nchini Ujerumani nao kwa upande wao wamesaidia miundombinu ya majengo kwa kujenga nyumba za walimu za muundo wa nyumba moja ndani ya tatu.

Amesema kutokana utajiri huo wa msaada wa vifaa hivyo vya masomo ya sayansi, shule hiyo imeamua kusaidia wanafunzi wa shule za jirani kuja kujifunza kwa vitendo hasa wakati huu wa likizo.

Amesema hali hiyo imeipunguzia shule hiyo mzigo hivyo kutumia fursa hiyo kujikita zaidi kusaidia waqnafunzi kuongeza uelewa, ambapo sasa wanafunzi wote wale wa bweni na kutwa hupata chakula shuleni hapo.


Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top