Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Na
EmanuelMadafa,Mbeya
Watu
watano wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria lenye namba za
usajili T.143 Ajr aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa
na Robert
Mwakibibi (37) mkazi wa Uyole .
Ajali
hiyo imetokea mnamo Des15 mwaka huu majira ya saa 11:45 asubuhi huko katika kijiji
cha Kantela-Ntokela, Kata ya Ntokela, Wilaya ya Rungwe, Mkoani mbeya katika barabara kuu ya mbeya/tukuyu.
Inadaiwa
kuwa Chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu katika mfumo wa breki wa gari hilo
hali iliyosababisha dereva huyo kumshinda na kupinduka ambapo Inadaiwa kuwa watu hao walikuwa
wanakwenda kuzika kijijini hapo
wakitokea jijini Mbeya
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema Waliofariki katika ajali hiyo ni
wanawake watatu na wanaume wawili ambao ni Sophia Omary (50) Mkazi wa Mbalizi Stela
Mwaluswaswa (38) mkazi wa Tunduma .
Wengine
ni Suzana Melele (31) mkazi wa
mbalizi Bulele Mwaipaja (48) Mkazi wa uyole na Jacob
Nyaluke (17) mwanafunzi kidato cha nne shule ya sekondari Mbozi misheni na
mkazi wa mbozi.
Aidha
katika ajali hiyo watu 32 wamejeruhiwa
kati yao wanaume ni 16 na wanawake ni 16 ambao wamelazwa katika
hospitali za misheni Igogwe na Makandana – Tukuyu.
Aidha
Dereva wa gari hilo alikimbia mara baada ya tukio na jitihada za
kumtafuta zinaendelea.
MWISHO.
|
Post a Comment