Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Askofu Kiongozi wa kanisa la Moraviani Tanzania, Alinikisa Cheyo |
Burudani |
Kuwasha mshumaa kuwakumbuka waliotangulia mbele za haki kutokana na ugonjwa huo. |
Mratibu wa Ukimwi Jiji la Mbeya,Happy Luteganya,akisoma risala |
Mwandishi wa habari kutoka Fahari News blog akipima afya yake |
NaMwandishi
wetu,Mbeya
WATU
wanaoishi na virusi vya Ukimwi Mkoa wa Mbeya, wamezitaka Asasi na Taasisi
zinazojihusisha na mapambano dhidi ya ugonjwa huo kupigania
uwepo wa sheria mahususi ambayo itawalinda na mazingira hatarishi ya
zaidi yatakayotokana na utengenezaji wa
dawa za kufubaza virusi zilizochini ya kiwango.
Wito huo
ulitolewa Jijini Mbeya na mmoja wa watu
hao wanaoishi na virusi hivyo, Alfred Sanga, wakati akitoa ushuhuda wa namna
yeye na Mkewe, Aza Spea Sanga, walivyofanikiwa
kufuata masharti ya utumiaji dawa hizo za ARV na kuzaa mtoto asiye na
maambukizi.
Akizungumza
mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, Askofu
Kiongozi wa kanisa la Moraviani Tanzania, Alinikisa Cheyo, ambapo kwa Jiji
hilo, yalifanyika kwenye uwanja wa Mbata, Sanga amesema kitendo hicho
kinawaweka katika mazingira hatarishi zaidi.
Kwa upande
wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Askofu Cheyo amesema kuwa licha ya
kwamba viwango vya maambukizi kupungua mkoani Mbeya kutoka
asilimia 9.2 katika utafiti wa mwaka
2008 hadi kufikia asilimia 9.0 katika utafiti wa mwisho wa mwaka 2012.
Hata hivyo,
alitaka jitihada zaidi za serikali na wadau wa ugonjwa huo kuhakikisha
wanawafikia vijana wengi walio shule ili kuwapa elimu ya kutosha juu ya maambukizi
na kujikinga na Ukimwi , tofauti na sasa ambapo ni asilimia 65 tu ya wanafunzi
wamefikiwa.
Awali akisoma
risala katika maadhimisho hayo, Mratibu wa Ukimwi Jiji la Mbeya,Happy
Luteganya, alisema licha ya jitihada mbalimbali za kuelimisha jamii juu ya ugonjwa
huo, bado kuna changamoto nyingi.
Aidha,
Luteganya alisema changamoto nyingine inayokwaza zaidi vita dhidi ya mapambano
dhidi ya Ukimwi ni kutokana na program zake kuwa tegemezi, huku kwa Mkoa wa
Mbeya ukiwa na asasi 36, ambapo 15 kati ya hizo ndio hutoa taarifa.
Post a Comment