Shirika la habari la BBC linazindua
tuzo kwa heshima ya aliyekuwa mtangazaji wake Komla Dumor, mwaka mmoja
baada ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 41.
Komla Dumor alikuwa mwandishi na mtangazaji mwenye kipaji cha
kipekee kutoka nchini Ghana huku akisifika sio Ghana pekee bali Afrika
na duniani kote.
Aliwakilisha Afrika kama bara lenye kujiamini na lenye wajasiri amali wengi.
Kupitia
kwa kazi yake ya uandishi na kusimulia taarifa kwa wengi, Komla
alifanya kazi kwa kujitolea sana kutoa taswira tofauti kuhusu Afrika kwa
dunia nzima.
Shirika la BBC limejitolea kuandeleza kazi ya Komla.
Tunajivunia sana kama BBC kutangaza tuzo ya uandishi wa habari kwa heshima ya aliyekuwa mwandishi mahiri wa BBC Komla Dumor
Tuzo
hio itakuwa inatolewa kwa wandishi wenye kipaji wanaoishi barani Afrika
na kufanya kazi barani humo. Sharti ni kwamba watakuwa wana kipaji cha
hali ya juu kusimulia taarifa kuhusu bara la Afrika na pia wawe
wanalenga kuwa mahiri katika siku za usoni.
Kupitia kwa tuzo
hio,BBC itaweza kumleta mshindi katika shirika hilo kupata ujuzi wa kazi
na kusimulia taarifa kuhusu Afrika kwa dunia nzima kwa kipindi cha
miezi mitatu mjini London.
Mshindi pia atapata fursa ya kutangaza
kwenye televishini , redio na kuandika taarifa ambazo zitachapishwa
kwenye mtandao kwa mashabiki milioni 265 wa BBC kote duniani.
mwisho
Post a Comment