Waamuzi waliosimamishwa
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na watu wengine
watahojiwa na ujumbe huo. Matokeo ya uchunguzi huo yatatangazwa na FIFA baada
ya shughuli hiyo kukamilika.
Tunaendelea kuwahimiza
wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za maadili za TFF,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA katika utendaji wao. FIFA
itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi ambao inaufanya.
Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)l imepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo tena kortini
kwa kesi dhidi ya uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), jambo
ambalo linaweza kuathiri ushiriki wa timu za Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa
Afrika, na Kombe la Shirikisho.
Mwishoni mwa mwaka jana,
TFF ilihadharisha juu ya masuala ya mpira wa miguu kupelekwa mahakamani, kwani
kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni
kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya
mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.
Kutokana na hali hiyo,
TFF iliiandikia barua ZFA kutaka mgogoro huo uondolewe kortini na yenyewe
kuridhia kuwa tayari kupeleka ujumbe Zanzibar ili ukutane na pande
zinazohusika.
Pia TFF ilisema timu za
Tanzania Bara zisingeruhusiwa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015
iwapo kesi hiyo ingeendelea kuwepo kortini na kutaka iondolewe bila masharti
yoyote.
ZFA iliithibitishia TFF
kuwa kesi hiyo imeondolewa kortini bila masharti, hivyo timu za Tanzania Bara
kuruhusiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ni muhimu suala hilo likashughulikiwa haraka ili kutohatarisha
ushiriki wa timu za KMKM na Polisi kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF).
Post a Comment