Abiria wakiwa kwenye foleni kusubiri usafiri wa shirika la Ndege la Fast Jet |
Na Mwandishi Wetu, Mbeya.
KUFUATIA kwa tatizo la kuchafuka kwa
hali ya hewa iliyoambatamna na ukungu, iliyojitokeza jJijini Mbeya jana hivyuo
kusababisha ndege ya abiria ya Fastjet kushindwa kutua katika Uwanja wa
Kimataifa wa Songwe, leo abiria wamejikuta wakipanga foleni ndefu ya kuingia
ndani ya uwanja hali ambayo imeonekana kuwakera baadhi ya wasafiri.
Mbali na kero hiyo, pia wasafiri
walilazimika kuwahi kufika kwenye uwanja huo na kukaguliwa mapema ili
kuondokana na hali ya usumbufu wakati wa kuingia ndani ya uwanja huo.
Fahari News, imeshuhudia foleni
ndefu ya habaria wakiwa wanasubili kuingia kwenye chumba cha ukaguzi huku
baadhi yao wakionekana kukerwa na hali hiyo.
“Hii sasa imekuwa shida kwani
mtu umefika mapema lakini mpaka sasa tupo kwenye foleni ambayo haieleweki
itamalizika muda gani,” alisema abiria ambaye ahakutaka jina lake liandikwe.
Alisema, ikumbukwe kwamba
abiria huwa anawahi kufika uwanjani ili kukamilisha taratibu mapema na
kupumzika lakini sasa angalia foleni ni ndefu na mtu anaweza jikuta akichoka
kabla ya kuanza safari ni vema serikali ikaharakisha mpango wa ufungaji wa Taa
kwenye uwanja huo.
“Kama Taa zingekuwepo abiria ambao
walipaswa kusafiri jana asubuhi na mchana wangeondoka usiku wa saa nne hivyo
kupunguza msongamano uliojitokeza hivi leo.”alisema
Aidha, akizungumzia hilo, Mratibu wa
shughuli za ndege Kampuni ya Fastjet Mkoa wa Mbeya, Omary Idrissa, alikiri
kujitokeza kwa msongamano mkubwa uwanjani lakini suala hilo limerekebishika kwa
kuwaomba abiria ambao walipaswa kuondoka na ndege ya jana kuondoka kesho.
“Mpaka sasa tumeweza kulitatua
tatizo hili kwani baadhi ya abiria wameondoka na ndege ya asubuhi wengine
wataondoka leo jioni na wale ambao walitakiwa kuondoka jana watatarajia
kuondoka kesho kwani waliobaki ni wachache ,”alisema.
Mwisho
Post a Comment