Na Emanuel Madafa,Mbeya
ZAIDI
ya ibiria 131 waliokuwa wakisafiri na shirika la ndege la Fast Jet kutoka Dar
es salaam wameshindwa kutua katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe jijini Mbeya kutokana na hali ya hewa
kutoka nzuri.
Akizungumzia
tukio hilo Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe, Valentine Kadera, alikiri ndege hiyo kushindwa kutua
kwenye uwanja huo, hivyo kulazimika kugeuza Jijini Dar es Salaam
kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.
Ameseema
endapo hali hiyo ya hewa ingekuwa vizuri ndege hiyo ingetua kama kawaida kwani
hapa kuwa na tatizo lolote la kiufundi tofauti na hali hiyo ya hewa kuwa mbaya.
Akizungumzia
tatizo hilo, mratibu wa shughuli za ndege kutoka Kampuni ya Fastjet Mkoa wa
Mbeya, Omary Idrisa, alisema ndege hiyo imeshindwa kutua kutokana na hali ya
hewa kuwa mbaya hivyo kulazimika kugeuza kurudi Jijini Dar es Salaam mpaka
kesho mchana.
Aidha,
Mratibu huyo, aliiomba serikali kukamilisha miundombinu ya Taa katika uwanja
huo kwani ndege hiyo ilikuwa na uwezo wa kutua usiku majira ya saa nne au
alfajiri ya saa 11 na saa moja asubuhi kama miundombinu hiyo ingewezeshwa.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment