mama mlezi wa kituo hicho Anah Kasire akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhiwa msaada huyo. |
Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Nice Catering company limited yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam Yohana Sonero akikabidhi fedha kwa watoto hao ambazo zilihitajika kwa ajili ya karo ya shule. |
Baadhi ya wafanyakazi wakihesabu fedha zilizochangwa kwa muda na wafanyakazi hao |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
JUMLA ya shilingi milioni 1.4 zimetolewa na Kampuni ya Nice
Catering ya Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia watoto yatima ambao walikuwa
wameshindwa kuendelea na masomo kwa mhula huu wa pili.
Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo,Yohana
Sonero, kwa Mama mlezi wa kituo hicho cha
kulea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi cha Malezi ya Huruma kilichopo
eneo la simike Jijijini Mbeya,ameiitaka jamii kujenga tabia ya kusaidia watoto
bila ya kutanguliza maslahi yao binafsi.
Amesema nivema Wadau na Taasisi mbalimbali zikatambua kuwa suala la kutoa misaada kwa
watu wasio jiweza ni moyo, hivyoamekemea tabia ya ya watu kugeuza misaada hiyo
kuwa sehemu ya kujitangaza au kujinufaisha kwa maslahi binafsi.
Amesema, kumeibuka tabia ya watu kuamua
kuanzisha vituo vya kulelea watoto yatima kwa lengo la kupata misaada
mbalimbali kutoka kwa wafadhili na wadau lakini imekuwa haiwafikii walengwa husika.
Aidha kutokana na hali amewataka wadau
mbalimbali kuto lifumbia macho suala hilo badala yake wajikite katika kusaidia
makundi ya aina hiyo ambayo yanahitaji msaada mkubwa toka kwa jamii.
Akipokea msaada huo mama mlezi wa kituo hicho
Anah Kasire ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo, ambao umefika kwa wakati
kwani kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa fedha hususani
ada za wanafunzi wa sekondari.
Mwisho.
Post a Comment