![]() |
| Peter Nzito |
Stori: Saimeni Mgalula,Mbeya
Kijana mmoja Stivini Nzito (28) Mkazi wa mji wa Uyole,Kata
ya Igawilao Wilayani Mbeya Mjini Mkoani hapa,amesimulia jinsi maajabu
yalivyotaka kumtokea baada ya kupotea kwa mdogo wake Peter Nzito katika
mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na Paparazi wetu hivi karibuni Nyumbani
kwake,kijana huyo alisema hofu kubwa ni kabla ya kupotea kwa mdogo
wangu,alipotea jirani yangu ambaye hakumtaja kwa jina iia alikuwa ni mfanya
biashara wa kuuza nguo kwa kutembeza .
‘’Ambaye naye alipotea kama mdogo wangu na akaja kupatikana
Tunduma akiwa mikononi mwa polisi huku akiwa ni marehemu na cha kushangaza
maiti hiyo ilizikwa na polisi kutokana na kutotambulika kwa mara moja’’.
Baada ya kusikia hivyo kuwa kuna mtu amezikwa na jeshi la
polisi kutokana na kutotambulika kwa ndugu zake ilibidi waende kuangalia ndipo
polisi iliwaonesha nguo ambazo alikuwa amevaa hapo ndipo alipogundulika kuwa ni
yeye .
Aliendelea kuelezea mkasa huo Kijana huyo alisema ,Mdogo
wangu tumetafuta sana kwa kushirikiana na jeshi la polisi bila ya mafanikio na
ndipo tuliamua kwenda kwa Mganga wa kienyeji ili tujue mahali alipo ni salama
na ni sehemu gani.
‘’Nilikwenda kwa Mganga huyokatika kijiji cha Chimbuya
ambacho kipo katika Wilaya ya Momba mkoani hapa,Mganga hakutoa majibu ya mahali
ambapo yupo ila aliniambia kuwa yupo hai ila ni kukazana tu kumtafuta na hupo
hapa hapa Tanzania.
Mara baada ya mganga huyo nilikwenda kwa mganga mwingine
katika kijiji cha Anseketwa kilichopo katika Wilaya hii ambaye anasema kuwa
walishindana kutokana na mashart aliyompa ya kukata kidole chake cha mwisho katika
mkono wa kushoto ili kuipa mizimu yake nyama.
![]() |
| Mdogo wa Nzito |
Kijana huyo aliendelea kueleza kwamba baada ya mimi kuona
hivyo niliamua kukataa mashart ndipo mganga alinitoza faini ya shilling laki
mbili huku akisema kuwa atachukuwa kwa muda wake pesa hizo mpaka atakapo maliza
deni lake,
Aliongeza kuwa baada
ya maneno ya Mganga nilitoka na kurudi nyumbani mara baada ya kufika
nyumbani kuna pesa nilikuwa nazo
nikakuta hazipo ghafla ukatokea mzimu ambao uliniambia kuwa si nilikwambia kuwa
nitachukuwa kwa muda wangu sasa ndo nimechukuwa ukapotea.
‘’Kutokana na hile hali ya kutokewa na mzimu niliamua kuacha
kwenda kwa waganga wa kienyeji mara baada ya mzimu huo kutaka kumzuru kwa
kukataa shart ambalo aliambiwa na Mganga juu ya kuchangia mashetani yake ndipo
yamsaidie kumwonyesha.
Pia ,alisema pamoja na mdogo wangu kuto kuaga kwa rafiki
yake yeyote hapo ndio panapo umiza kichwa sana na kusababisha nyumbani kuwe
kama kuna msiba hivyo basi kwa yeyote ambaye atakuwa anafahamu alipo au alishawahi kumuona sehemu yeyote apige
simu no 0757162769








Post a Comment