![]() | |
| Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi. |
POLISI
Mkoani Mbeya, imetoa ufafanuzi kufuatia vurugu zilizofanywa na wananchi wa Mji
mdogo wa Mbalizi na baadhi ya askari wa jeshi la wananchi kikosi cha 44KJ cha
Mbalizi, ambapo vurugu hizo zilisababisha kifo cha askari mmoja.
Aidha imeelezwa kuwa ,
vurugu hizo hazikusababishwa na ugomvi wa kimapenzi kama
ulivyoelezwa na kuenezwa na baadhi ya watu bali ni ugomvi ambao uliwahusisha
baadhi ya vijana raia na wanajeshi wa kikosi cha Mbalizi 44KJ baada ya
mwanajeshi mmoja aliyepanga ulaiyani kuibiwa mali zake.
Akimtaja
askari huyo aliyeuawa katika vurugu hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi, amesema ni marehemu mwenye namba FT 1096619 Mwaka Ahadi
kutoka kikosi namba 825 cha JKT Mtabila kilichopo Mkoani Kigoma.
Aidha,
amesema kuwa askari huyo alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika
hospitali ya Jeshi ya Mbalizi kikosi cha 44KJ.
Akielezea
sababu za vurugu hizo, Msangi amesema, viashiria vya kutokea kwa vurugu hizo,
vilianza kutokea siku ya Jumanne ya tarehe 3 mwezi February, 2015 baada ya
kukamatwa kwa vijana nane na kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya
kipolisi ya Mbalizi kwa tuhuma za wizi wa radio na televisheni.
Amesema,
kwa mujibu wa taarifa hizo, inasemekana kwamba katika msako huo vijana nane
walikamatwa kati ya tisa na kufikishwa katika kituo cha polisi.
Amesema,
hivyo wananchi walipowaona wanajeshi kwenye eneo lao walianzisha vurugu
zilizoambatana na uvunjifu wa amani .
Amesema, wakati
pande hizo mbili zikitoa maelezo yao ndipo kulipozuka mzozo mkubwa
hivyo kuibukatena kwa vurugu zilizovuta hisia za watu ambao walifika na
kuzua taflani.
Amesema,
katika vurugu hizo askari mmoja wa jeshi la wananchi, Ahadi Mwaka aliumizwa
kwenye sehemu ya kichwa na katika kidevu hivyo kukimbizwa hospitali ya jeshi ya
Mbalizi na kupoteza maisha wakati akipatiwa matibabu hayo.
Amesema,
vurugu hizo zilisababisha hali ya amani kutoweka kwenye eneo hilo, hivyo
polisi kulazimika kuongeza nguvu zilizosaidia kuwatuliza wananchi ikiwa na
kuwaondoa hofu iliyokuwa ikiwatawala kwamba huenda wanajeshi wakawavamia
na kuwapiga.
Hata
hivyo, katika vurugu hizo hakuna raia aliyeumia lakini baadhi ya watu
wamelalamika kuharibiwa mali zao na kwamba uchunguzi unaendelea.
Mwisho.







Post a Comment