Wakati
mwanamziki wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz akiendelea kupepesa macho na
kutikisa masikio kukanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na
mwingizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ukaribu wao bado unatia mashaka
na kuendeleza sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wapambe wao.
Japo kuwa Ommy alielezakuwa yeye na Wema ni marafiki toka kitambo
kabla hata ya wema kuwa na mahusiano na mwanamziki Diamond, lakini hii
sasa imezidiii.
Mbali na kuonekana pamoja sehemu mablimbali za starehe toka Ommy
atoke Marekani, hili la kupikiwa na kupakuliwa nyumbani kwa Wema tena
mida ya usiku ndio limezidi kuchochea hisia kuwa wawili hao
wanamahusiano zaidi ya USHKAJI.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwanadada Wema ambae
na folloers zaidi ya laki nne , alibandika picha hiyo hapo juu
akionekana kumpakulia chakula ambacho alijisifia ni kizuri na amekipika
mwenyewe na kumtania Ommy kuwa alikuwa analeta pozi kwenye kula.
“Dat moment anapokuja home and umepika chakula alafu analeta pozi at first then unashangaa anaenda sahani mbili.... Talk About Good Food Made Real Good”- Wema aliandika mara baada ya kutupia picha hiyo.
Japo kuwa hadi sasa mwanadada Wema Sepetu ajajitokeza kukataa au
kukubali juu ya yeye kuwa na mahusiano na Ommy lakini idadi kubwa ya
wampambe wake mitandaoni na ifagilia sana hii “Couple”.
Tuvute subraaa.
Mzee wa Ubuyu
|
Post a Comment