Kuna taarifa
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuelezea kwamba kutakuwa na mgomo wa
wafanya biashara wa mafuta nchini, na kwa hiyo kutakuwa na uhaba wa mafuta ya
jamii ya petroli.
Aidha, taarifa hizo
zinawachochea watumiaji wa bidhaa hizo kununua kwa wingi ili kuepuka
usumbufu.
EWURA inapenda
kuutaarifu umma kwamba taarifa hizo si za kweli, hakuna mgomo wala tatizo
lolote linaloweza kuhatarisha upatikanaji wa mafuta nchini, na kwamba nchi ina
akiba ya kutosha ya mafuta, na hakuna haja ya wadau kuwa na wasi wasi.
Umma unakumbushwa pia
kuzipuuza taarifa za namna hiyo kwa sababu ni za upotoshaji na zinalenga
kuvuruga hali ya utulivu wa soko la mafuta nchini. Ikumbukwe pia kwamba ni
EWURA tu yenye mamlaka ya kisheria ya kuutaarifu umma juu ya hali ya soko la
mafuta na upatikanaji wa bidhaa zake.
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano, EWURA.







Post a Comment