| Moja ya Vyumba vya madarasa vilivyo athiriwa vibaya na mvua hizo. |
| Wakazi wa eneo la Ilemi jijini Mbeya wakiwa juu ya paa za nyumba zao wakijaribu kufanya ukabati mdogo baada ya nyumba zao kuharibiwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali |
| Mwanafunzi wa shule ya msingi Ilemi Darasa la Tano ambaye aliangukiwa na ukuta akipelekwa hospital kwa matibabu zaidi. |
Mvua za
masika zinazoendelea kunyesha nchini Tanzania leo hii zimezua balaa baada ya
mvua kubwa iliyoambatana upepo mkali kunyesha katika maeneo mbalimbali jijini
Mbeya na kuleta maafa. Kati ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo ni pamoja na
Ilemi jijini Mbeya ambapo takribani kaya 40 pamoja na shule zimeezuliwa, huku
wanafunzi wawili wa shule ya msingi Ilemi wakijeruhiwa kwa kuangukiwa na kuta
za shule hiyo.
Mashuhuda
wa mvua hiyo iliyonyesha kwa karibu dakika 20 mchana majira ya saa nane
wameeleza kuwa mvua hiyo iliambatana na upepo mkali ambao uliweza kuangusha
kuta pamoja na miti na kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo. Kuhusiana
na shule zilizoathiriwa na balaa hilo, Vyumba vya madarasa, ofisi na vyoo
vimeezuliwa na upepo na baadhi ya kuta kudondoka ambapo Afisa Elimu jiji la
Mbeya kwa shule za msingi, Auleria Lwensa msingi ambaye alifika katika eneo la
tukio amewataka waalimu na wanafunzi kuendelea kuyatumia madarasa na ofisi
ambayo hayajaathiriwa.
Pamoja na hayo bi. Auleria amesema kuwa shule
haitafungwa na badala yake masomo yataendelea huku ukifanywa utaratibu na bodi
ya shule ili kuwezesha ukarabati wa majengo hayo huku akiwataka wakazi wa
maeneo hayo kupeana msaada unaowezekana kwa zile familia zilizoathirika na
janga hilo kwakuwa ni jambo la dharura.






Post a Comment