Mshambuliaji machachari wa klabu ya
Yanga, ameiomba klabu yake kumlipia deni analodaiwa benki ili aweze
kucheza kwa bidii na kuwa mfungaji bora.
Ngasa aliamriwa kulipa
deni la Sh 45 milioni kwa kosa la kujiunga na Yanga bila kufuata
utaratibu akitokea Simba, hivyo , kwa makubaliano, analazimika kukatwa
Sh500,000 (wastani wa dola 280) kila mwezi kutoka katika sehemu ya
mshahara wake anaoupata kutoka Yanga ili kulipa deni.
Kwa mujibu
wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, benki , baada ya
kukata 500,000, ililazimika kuchukua mshahara wote wa Ngasa katika miezi
ya hivi karibuni ili kufidia deni analodaiwa baada ya uongozi uliopita
wa klabu hiyo kushindwa kupitisha benki mshahara wake benki kwa muda
unaokisiwa mwaka mmoja, hivyo kutolipa kwa mujibu wa makubaliano na
benki kulazimika kumuacha mchezaji huyo bila senti.
Ngasa
aliripotiwa kusema kuwa hali yake ya kifedha “financial status” ni mbaya
na kushindwa kucheza vizuri, na kuiomba Yanga kuangalia namna ya
kumsaidia kulipa ili aweze kubakiwa na fedha za kutoka.
“Tutakaa na Ngasa tuangalie namna ya kumsaidia”.
“Licha
ya matatizo aliyonayo, ameonesha kuwa ni mchezaji anayejituma na magoli
mawili aliyofunga hivi karibuni na kutupa ushindi wa 2-0 dhidi ya
Mtibwa Sugar katika ligi kuu inaonesha anavyoithamin i timu yake”,
alisema Muro.
Kutokana na makato yanayomkabili, Ngasa, ambaye
mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu wa ligi, alitangaza kuachana na
Yanga ili akacheze mpira nje ya nchi, lakini klabu yake imesema
itamuongeza mkataba mwingine baada ya mazungumzo ya hivi karibuni.BBC






.jpg)
Post a Comment